Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Michezo Kimeumana: Yanga wamtengea Tshabalala Mil 150, mshahara Mil 7
MichezoTangulizi

Kimeumana: Yanga wamtengea Tshabalala Mil 150, mshahara Mil 7

Mohammed Hussein
Spread the love

 

IKIWA imebakia miezi miwili kumaliza kwa mkataba wake ndani ya klabu ya Simba, beki wa kushoto na nahodha msaidizi wa kikosi hiko, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ huenda akatimkia kwenye klabu ya Yanga baada ya kumtengea kiasi cha Sh. 150 milioni kama ada ya uamisho na mshahara wa Sh.7 milioni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezaji huyo mwenye miaka 26, amedumu kwenye kikosi cha Simba kwa kipindi cha miaka saba toka 2014 alipojiunga akitokea Kagera Sugar.

Taarifa ambayo MwanaHALISI Online imezipata kutoka kwenye chanzo cha kuamainika, kimeeleza kuwa Tshabalala ataondoka Simba kufuatia kukubaliana na Yanga na kuitumikia timu hiyo msimu ujao.

“Tshabalala ameshamalizana na Yanga kila kitu na wanasubiri msimu uishe wamtangaze, njia pekee ya Simba kumbakisha labda Simba wampe hela nyingi ili aweze kuwarudishia Yanga pesa yao,” kilisema chanzo hiko.

Aidha chanzo hiko kimeeleza kuwa tayari Yanga wameshafunga hesabu na mchezaji huyo kufuatia uongozi wa Tshabalala kukubali kiasi cha fedha Sh. 150 milioni kama ada ya uamisho na mshahara wa Sh. saba milioni kwa mwezi.

“Ndugu yangu Tshabalala amevuta milioni 150 kutoka Yanga na watampa mshahara wa milioni saba kwa mwezi kwa mkataba wa miaka miwili,” kiliongezea chanzo hiko.

MwanaHALISI Online lilijaribu mkutafuta Meneja wa mchezaji huyo, Herry Mzozo kupitia namba yake ya simu ya mkononi majira ya saa 5:31 asubuhi lakini haikupokelewa.

Licha ya kutopokelewa kwa simu hiyo lakini siku za hivi karibuni meneja wa mchezaji huyo kupitia mahojiano yake aliyofanya katika chombo kimoja cha habari hapa nchini, alinukuliwa akisema kuwa timu itakayomtaka Tshabalala ijue thamani ya mchezaji huyo kwa sasa ni milioni 100 na mshahara milioni usipungue milioni 8.

“Niwaraisishie thamani ya mchezaji ni shilingi milioni 100 kwa mwaka ya usajili, mshahara milioni 10 kwa mwezi ikipungua shilingi milioni nane,” alinukuliwa meneja huyo.

Taarifa za mchezaji huyo kutimkia Yanga zinachagizwa na kauli ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Yanga na Mkurugezi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Mhandisi Hersi Saidi ya kusema kuwa “Tutaendelea kuijenga Yanga msimu ujao ikiwemo kuvunja benki zinazowahifadhi watu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia ampandisha cheo RPC wa Dar

Spread the loveMKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amesema...

Habari za SiasaTangulizi

Wanachama 384 CUF watimkia Chadema, Mbowe awapokea, Kambaya ndani…

Spread the loveJUMLA ya wanachama 384 wanachama wa Chama cha Wananchi CUF...

error: Content is protected !!