May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Real Madrid, Chelsea vitani nusu fainali UEFA leo

Spread the love

 

KLABU ya Real Madrid itashuka dimbani leo kuwaalika Chelsea kwenye nusu fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA) kwenye mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Alfred Di Stefano. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Nusu fainali hiyo ya kwanza itachezwa majira ya saa 4 kamili usiku huku Real Madrid ikiwa na rekodi nzuri mbele ya Chelsea kwenye michuano hiyo.

Katika michezo mitatu waliokutana vigogo hao wa soka barani Ulaya, Chelsea amefanikiwa kuibuka na ushindi mara mbili na kutoka sare mchezo mmoja.

Mara ya kwanza Chelsea kukutana na Real Madrid ilikuwa Mei 1971 kwenye michuano ya Kombe la Ulaya ambapo sasa hivi ni (UEFA) na Chelsea ilifanikiwa kuiondoa Real Madrid kwa jumla ya mabao 3-2 katika michezo yote miwili.

Chelsea imefanikiwa kufuzu hatua hii ya makundi baada ya kuwaondoa klabu ya FC Porto kutoka Ureno kwa jumla ya mabao 3-0 katika michezo miwili.

Kwa upande wa Real Madrid wao walifuzu hatua hii ya robo fainali mara baada ya kuwasukuma nje klabu ya Liverpool kwa jumla ya mabao 3-1.

error: Content is protected !!