May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Askofu TAG akerwa na mila za kudharau wanawake

Askofu Mkuu wa TAG Dk.Barnabas Mtokambali akiwa anahubiri katika ibada ya kuwasimika viongozi mbalimbali wa kanisa hilo.

Spread the love

 

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Tanzania Asembless Of God (TAG), Dk. Barnabas Mtokambali, amekemea tabia ya mila za kudharau wanawake na kudhani hawawezi kupewa majukumu makubwa katika nchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

“Nataka niwakemee watu wote waliopo Tanzania, kuachana na tabia ya kudhani kuwa, mwanamke hawezi kuongoza.”

“… badala yake wanatakiwa kutambua na kuamini, mwanamke anao uwezo mkubwa wa kuongoza na wakati mwingine anaweza kuwa na busara kuliko hata mwanaume,” amesema Askofu Mtokambali.

Ametoa karipio hilo leo tarehe 27 Aprili 2021, wakati wa ibada maalum ya kuwasimika viongozi wakuu wa kanisa hilo – Askofu wa Jimbo la Dodoma, Makamu Askofu wa Jimbo la Dodoma, Katibu wa Jimbo pamoja na Mtunza Hazina jimbo hilo- iliyofanyika katika Kanisa la T.A.G Upendo Revavil, Area D.

Katika ibada hiyo Askofu Dk. Mtokambali amesema, Tanzania imepata bahati ya kuwa na rais mwanamke ambaye amepatikana kwa mujibu wa Katiba ya nchi.

Amesema, Rais Samia ni kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza kwa kuwa, anao uelewa na elimu ya uongozi.

Kiongozi huyo wa kiroho amesema, wanasiasa wanapaswa kufanya siasa zenye kuhamasisha upendo na mshikamano kwa maslahi mapana ya Taifa.

“Kuna kila sababu ya kuwa na siasa safi ambazo hazilengi kuwabagua Watanzania,” amesema Askofu Mtokambali.

error: Content is protected !!