May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kim Poulsen mshauli mkuu soka la vijana

Kim Poulsen

Spread the love

 

ALIYEWAHI kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars,’ Kim Poulsen anarejea tena nchini na kuwa mshauri mkuu wa soka la vijana kwa timu za Taifa chini ya umri wa miaka 17 na 20. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Kocha huyo raia wa Denmark ambaye aliondoka nchini 2018, baada ya kuajiliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kama Mkurugenzi wa maendeleo ya soka nchini na kuhudumu kwenye nafasi hiyo kwa mafanikio.

Taarifa za ndani kutoka TFF zinaeleza kuwa Poulsen atarejea tena nchini kwa ajili ya kuwa mshauri wa timu za Taifa za vijana, tofauti na taarifa zinazosambaa ya kuwa anakuja kuchukua mikoba ya Ettiene Ndayilagije ambaye anakinoa kikosi cha Taifa Stars kwa sasa.

Poulsen si mgeni kwa soka la vijana hapa nchini, kwani mwaka 2011 hadi 2012 alishawahi kukinoa kikosi cha Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 19 na baadae akapandishwa kuinoa Taifa Stars.

Pengine ujio wa kocha huyo katika nafasi ya ushauri itakuwa chachu ya kuendelea kufanya vizuri kwa timu za Taifa za vijana ambazo mbili zimefanikiwa kufuzu michuano ya kombe la mataifa Afrika ‘AFCON’ chini ya umri wa miaka 17 na 20.

Tayari timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ambayo ipo chini ya kocha Jamhuri Kihwelo, inatarajia kuondoka hivi karibu kuelekea nchini Mauritania kwa ajili ya michuano ya AFCON na watashuka dimbani kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Ghana tarehe 16 Februari 2021.

error: Content is protected !!