May 21, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Tembo, nyati wazua taharuki Selous’

Tembo wakiwa katika Hifadhi

Spread the love

KUTOKANA na wanyama kuongezeka katika Hifadhi ya Mbuga ya Selous, tembo na nyati wanatajwa kuzua taharuki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatatu tarehe 8 Februari 2021, na Vita Kawawa, Mbunge wa Namtumbo (CCM), akiitaka wizara ya maliasili na utalii ina mpango gani kuhakikisha wanyama hao wanakuwa mbali na wananchi.

”Kumekuwa na ongezeko la wanyamapori katika Hifadhi ya Mbuga ya Selous, na sasa tembo na nyati wanavamia mashamba pamoja na makazi ya wanavijiji na kuleta taharuki.”

“Je, serikali inaweza kuwarudisha wanyama hao porini mbali zaidi na wananchi?” ameuliza.

Akijibu swali hilo, Mary Masanja, naibu waziri wa wizara hiyo, amesema, wizara hiyo imeandaa na inatekeleza mkakati wa kitaifa wa kusimamia utatuzi wa migongano baina ya binadamu na wanyamapori.

Na kwamba, wizara hiyo inaendelea kukamilisha utaratibu wa kuweka alama katika shoroba na mapito ya wanyamapori ili kuimarisha uhifadhi wake, pia kuendelea kufanya utafiti na kueneza matumizi ya mbinu mbadala za kujikinga na wanyamapori waharibifu hasa tembo.

“Baadhi ya mbinu hizo ni: matumizi ya pilipili, mafuta machafu (oil) na mizinga ya nyuki; na kutoa mafunzo kwa askari wa wanyamapori wa vijiji.

“Wizara imekuwa ikiendelea kufanya doria za msako kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu, ambapo katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2020, zilifanyika doria za msako zenye jumla ya siku 133 katika vijiji vya Wilaya ya Namtumbo,” amesema Mary.

Mary amesema, jambo jingine ni wizara inafanya ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya mbinu za kujikinga na wanyamapori wakali na waharibifu, na kwamba jumla ya wananchi 2,303 walipata elimu katika vijiji 42 vya Wilaya za Namtumbo na Tunduru.

“Pia tunaimarisha vituo maalum vya doria za kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu katika Kanda za Kalulu na Likuyu-Sekamaganga,” imeelezwa.

error: Content is protected !!