
YUSTINA Rahhi, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), ameapishwa leo Jumatatu tarehe 8 Februari 2021, kuchukuna nafasi ya Martha Jecha Umbulla aliyefariki dunia tarehe 21 Januari 2021. Anaripoiti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
Rahhi ambaye kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho, alishika nafasi ya tatu, huku marehemu Umbulla akishika nafasi ya pili, ameapishwa na Job Ndugai, Spika wa Bunge.
Umbulla alifariki nchini India katika Hospitali ya HCG Mumbai.
Kifo cha mbunge huyo aliyezaliwa tarehe 10 Novemba 1955, kilitangazwa na Spika Ndugai tarehe 21 Januari 2021.
“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Mkoa wa Manyara. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” alisema Spika Ndugai.

More Stories
Rais Samia apokea tuzo ya Babacar Ndiaye, amtaja Magufuli
Mbunge Ditopile awapigania wavuvi
Msajili wa vyama ampiga ‘Stop’ Mbatia NCCR-Mageuzi