December 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kilango aanzisha miradi kusaka kura Serikali za mitaa

Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango

Spread the love

 

MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM) ameazisha miradi ya viti vya kukodisha kwa ajili ya biashara kwenye kata 14 katika jimbo lake la Same Mashariki ambazo kila kata zimepatiwa viti 100. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Amesema atahakikisha pesa zinazopatikana zinawasaidia kwenye kampeni za wenyeviti wa vitongoji na vijiji ifikapo mwaka 2024 kusiwe na changamoto yoyote ya pesa wakati wa kampeni.

Pia amewagiza madiwani kutunza mradi huo wa kukodisha viti hili huwe chachu ya maendeleo katika serikali za mitaa lengo ni kuwanadi vingozi wao wa chama cha mapinduzi

Kilango amesisitiza kata itakayofanya vizuri 2023 atawaongezea mradi mwingine ili wajikite kutengeneza pesa ambazo zitawanufaisha kwenye chaguzi ndogo ndogo na kuondoka na dhana za kuomba pesa za kampeni.

Alisema moja ya malengo ya kuanzisha miradi hiyo ni kukisaidia CCM kutekeleza Ilani kushinda chaguzi zote za serikali ya mtaa na uchaguzi mkuu ambao utafanyika Agosti 2025

Pamoja na mambo mengine, Mbunge huyo ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za Same Mashariki ambazo sasa zimekabidhiwa wakandarasi na zinafanyiwa kazi.

error: Content is protected !!