Thursday , 25 April 2024
Home Kitengo Michezo NBC yamwaga mikopo ya mabasi kwa vilabu
Michezo

NBC yamwaga mikopo ya mabasi kwa vilabu

Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) ambaye ni mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara (NBC Premier League) imesisitiza kuhusu dhamira yake ya kuboresha zaidi ligi hiyo kwa kuendelea kuziwezesha timu zinazoshiriki ligi hiyo ili ziweze kujenga uwezo wa kujitegemea. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Dhamira hiyo imesisitizwa na Mkurugenzi wa Fedha wa benki hiyo, Waziri Barnabas mapema leo tarehe 15 Novemba, 2022 wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu wa kawaida wa 17 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) uliofanyika jijini Mwanza.

Mkurugenzi wa Fedha wa benki ya NBC, Waziri Barnabas akizungumza na washiriki wa Mkutano Mkuu wa kawaida wa 17 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) uliofanyika jijini Mwanza leo tarehe 15 Novemba, 2022.

“Sisi wadhamini wa ligi hii tunajivunia sana kuona ligi yenye ushindani na viwango bora vya kiuchezaji vinavyoendelea kuonekana kwenye ligi hii. Hii inatokana na timu zinazoshiriki ligi hii kuweza kusajili na wachezaji wazuri kutoka ndani na nje ya nchi sambamba na kuweza kuwahudumia vema wachezaji hao ikiwemo kuwapatia maslahi yao,’’ alisema.

Kwa mujibu wa Waziri, mbali na udhamini wa ligi hiyo benki hiyo imebuni mikakati mbalimbali inayolenga kufanikisha dhamira hiyo muhimu ikiwemo mikopo ya mabasi kwa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki ligi hiyo ili kurahisha usafiri kwa vilabu hivyo.

“Ligi hii inahusisha suala zima la usafiri kwa vilabu husika na wakati mwingine timu zinasafiri kwa umbali mrefu sana na hivyo kusababisha uchovu kwa wachezaji.

“Upatikanaji wa mabasi mazuri ya kisasa utasaidia kupunguza uchovu kwa wacheza ili waweze kuleta ushindani unaohitajika wakiwa viwanjani. Tupo kwenye hatua nzuri na hivi karibuni baadhi ya timu zitapatiwa mabasi yao,’’ alisema.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano Mkuu wa kawaida wa 17 wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) uliofanyika jijini Mwanza hii leo wakijadili mada mbalimbali wakati wa mkutano huo.

Waziri alitaja huduma nyingine kuwa ni pamoja na  utoaji wa Bima kwa wachezaji, benchi za ufundi na familia za wachezaji wote wa ligi hii ya NBC Premier League.

“Tunaamini kuwa Bima hizi ambazo tunazitoa kupitia kampuni washirika za Britam na Sanlam, zimekuwa chachu kubwa kwa kuwaondolea wachezaji hofu za kucheza kwa woga wakihofia kupata majeraha yanayoweza kuathiri ajira zao. Hili limechochea sana wachezaji wetu kuonyesha viwango vyao,” alisema.

Aidha, Waziri aliwaomba wadau hao wamichezo vikiwemo vilabu, viongozi wa mchezo huo na wachezaji mmoja mmoja kuhakikisha wanachangamkia fursa ya kuwekeza kwenye Hati Fungani ya NBC Twiga Bond ili waweze kunufaika na faida mbalibali zitokazo na Hati fungani hiyo.

“Kiasi cha chini cha ununuzi wa hati fungani hiyo ni TZS 500,000. Kupitia uwekezaji huu wahusika wataweza kupata riba kubwa ya 10% kwa mwaka, inayolipwa nusu mwaka katika kipindi chote cha miaka mitano hadi Novemba 2027. Kiwango cha riba kinacholipwa hakina punguzo la kodi. Hivyo nawakaribisha sana wadau wa michezo,”  alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!