August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kigogo Z’bar ataka mchakato Katiba mpya uendelee ulipoishia

Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Abdulhamid Yahya Mzee

Spread the love

NI Katiba mpya, Tume Huru ya Uchaguzi tu. Hivyo ndivyo unaweza kusema kutokana na walivyosema watoa maoni wengi waliofika mbele ya Kikosi Kazi cha Rais Samia Suluhu Hassan cha kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vya siasa. Anaripoti Selemani Msuya … (endelea)

Katika Kikosi hicho, viongozi waandamizi wa kisiasa na kiutendaji, wamepita na kushauri mchakato wa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, ufanyike mapema kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025.

Baadhi ya waliotoa maoni kuhusu Katiba na Tume Huru ni Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, Mwenyekiti mstaafu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva, Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, asasi za kiraia na wadau wengine.

Mahitaji ya Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi, yameendele’a kutawala na kupata msisitizo mkubwa, ambapo jana, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Abdulhamid Yahya Mzee alitaka mchakato wa Katiba Mpya uendelee ulipoishia. Kusoma habari hii kwa kina jipatie gazeti lako la RAIA MWEMA leo.

error: Content is protected !!