Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakili akina Mdee: Tupo hatua za mwisho kufungua kesi
Habari MchanganyikoTangulizi

Wakili akina Mdee: Tupo hatua za mwisho kufungua kesi

Spread the love

WAKILI wa Halima Mdee na wenzake, Edson Kilatu, amesema wako katika hatua za mwisho za kufungua kesi ya wabunge hao viti maalum, kupinga mchakato uliotumiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwafukuza uanachama. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wakili Kilatu ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 19 Julai 2022, akizungumza na MwanaHALISI Online, kuhusu hatua waliyofikia katika ufunguaji wa kesi hiyo.

“Tupo hatua za mwisho kufungua. Tukifungua tutakujulisha. Ahsante,” amesema Wakili Kilatu, alipokuwa anazungumza na MwanaHALISI Online.

Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, tarehe 8 Julai 2022, iliwapa siku 14 wabunge hao viti maalum 19, baada ya kukubali maombi yao ya kupata kibali cha kufungua kesi dhidi ya Chadema, ili kupinga mchakato wake uliotumika kuwavua uanachama, wakidai haukuwa halali.

Katika maombi yao, Mdee na wenzake 18, wanaiomba mahakama ifanye mapitio ya kimahakama, dhidi ya mchakato uliotumiwa na Chadema kuwafukuza ndani ya chama hicho, wakidai haukufuata sheria kwa kuwa hawakupewa nafasi ya kujieleza na ulikuwa wa upendeleo.

Mbali na Mdee, wabunge wengine viti maalum wanaopinga kufukuzwa Chadema, ni Jesca Kishoa, Ester Bulaya, Esther Matiko, Hawa Mwaifunga, Grace Tendega, Agnesta Lambart, Cecilia Pareso, Asia Mwadin Mohamed na Felister Njau.

Wengine ni, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Styella Siyao, Salome Makamba, Anatropia Theonest na Conchesta Lwamlaza.

Wabunge hao walivuliwa uanachama wa Chadema, tarehe 27 Novemba 2020, ambapo walikata rufaa katika Baraza Kuu la chama hicho, ambazo zilitupiliwa mbali Mei 2022.

Baada ya rufaa hizo kutupwa, Mdee na wenzake 18, walikwenda mahakamani kufungua maombi ya kupinga kuvuliwa uanachama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

error: Content is protected !!