May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kiburi cha DED Temeke, wizara yajitosa

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusabilo Mkwabibi

Spread the love

 

INOCENT Bashungwa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amewataka wanahabari kutulia wakati akifuatilia kitendo cha udhalilishaji kilichofanywa na Lusubilo Mwakabibi, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wiki iliyopita, Mwakabibi alimuweka chini ya ulinzi mwandishi wa habari wa ITV, Richard Steven kwa kuhoji ufafanuzi wa kero za wananchi.

Waziri huyo ametuma ujumbe wake kwa wanahabari kupitia ukurasa wake wa twitter akisem “Wizara ya Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo tunafuatilia malalamiko ya wadau wa tasnia ya habari juu ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusabilo Mkwabibi, kumuweka chini ya ulinzi mwanahabari. Tunaomba wanahabari wawe na Subira wakati tunafanyia kazi suala hili.”

Kauli yake imetanguliwa na za wadau mbalimbali wa habari, wakieleza kulaani kiburi cha mkurugenzi huo, huku wakitaka hatua stahili zichukuliwe.

Miongoni mwa waliolaani kitendo hicho ni Deodatus Balile, Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ambaye aliwataka viongozi kutambua umuhimu wa vyombo vya habari sambamba na kuheshimu waandishi.

“Mkurungezi wa Manispaa ya Temeke anapaswa kutambua kuwa, kazi hizi zinafanana, hakuna kazi nzuri iliyo bora kuliko yake na hatutamfungia mtu kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki wananchi wa Manispaa ya Temeke,” amesema Balile.

Innocent Bashungwa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Irene Meero, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC), ambaye alisema, Mkwabibi amefanya udhalilishaji mkubwa si tu kwa mwandishi huyo  pekee, bali  kwa tasnia nzima ya habari Nchini.

“Kitendo cha mkurugenzi huyo kukataa kutoa ushirikiako kwa wanahabari ni kuvunja sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 kifungu cha 7, ambacho kinampa mwandishi mamlaka ya kukusanya, kuchakata na kuchapisha Habari,” amesema.

Akielezea chanzo, Irene amesema mwandishi Steven wiki iliyopita alimpigia simu Mkurungezi Mwakabibi kuomba kwenda ofisini kwake kupata ufafanuzi kutokana na sitofahamu kati ya wananchi wa Mtaa wa Magogoni, Yombo Dovya baada ya manispaa hiyo kuanza ujenzi wa shule ya sekondari Lumo.

kutokana na sitofahamu, wananchi walijitokeza kuzuia ujenzi huo na kudai kuwa,  eneo hilo linamgogoro ambao upo mahakamani.

Maofisa wa serikali waliokuwepo eneo la tukio, walikataa kutoa ufafanuzi na kuelekeza maswali yote aulizwe mkurugenzi.

Mwandishi huyo alipompigia mkurugenzi huyo na kuomba kwenda ofisini kwake kwa ajili ya kupata ufafanuzi.

Hata hivyo, baada ya kupiga simu kupokewa na mkurungezi huyo na kisha kueleza dhamira yake,  mkurugenzi huyo alianza kutoa kauli za kejeli na dhiaka.

“Wewe ni nani unaweza kupiga simu? Unasema unataka kuja kuniona? wewe ni Nani?,” alihoji.

error: Content is protected !!