December 8, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Wavuvi kicheko, TAFICO kufufuliwa

Spread the love

 

SERIKALI imeeleza, ipo kwenye mpango wa kufufua Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 13 Aprili 2021, na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati akisoma Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mwaka wa Fedha, Ofisi za Waziri Mkuu 2021/2021.

“Serikali inachukua hatua madhubuti katika kukuza sekta ya uvuvi kwa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa sekta hiyo.

“Hatua hizo, zinatokana na ukweli kwamba, sekta ya uvuvi inao uwezo wa kutoa mchango mkubwa kwenye kukuza Pato la Taifa, kupambana na umaskini na tatizo la ajira,” amesema Waziri Majaliwa.

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Amesema, katika mwaka 2020/2021, serikali imeanza kulifufua shirika hilo ikiwa ni pamoja na taratibu za ujenzi wa meli na bandari ya uvuvi.

“Tayari upembuzi yakinifu wa awali kwa ajili ya ujenzi wa bandari umefanywa,” amesema.

error: Content is protected !!