May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Tozo za bandari kupitiwa upya

Bandari Dar es Salaam Tanzania

Spread the love

 

SERIKALI imeeleza, kwamba itafanya vikao na wadau wa bandari ili kuangalia tozo zinazotozwa baada ya kulalamikiwa na wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

“Vikao vya wadau ikiwemo wananchi katika visiwa vya Kasalazi, Yozu, Gembela na Soswa vitafanyika kwa lengo la kupokea maoni yao kabla ya kuidhinishwa kwa tozo mpya,” ameeleza Dk. Leonard Chamuriho, Wazara ya Ujenzi na Uchukuzi leo tarehe 13 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma.

Dk. Chamuriho ametoa kauli hiyo baada ya James Shigongo, Mbunge wa Buchosakutaka kujua, ni lini serikali itaacha kutoza wananchi Sh. 600, wakati wa kuingia na kutoka bandarini katika visiwa vya Kasalazi, Yozu, Gembela na Soswa kwa kisingizio cha uwekezaji?

Dk. Chamuriho amesema, kiwango cha tozo ya abiria wanaopita katika bandari ndogo zilizopo katika maeneo mbalimbali ya mwambao wa bahari na maziwa, ni Sh. 600.

“kama ambavyo imeainishwa katika kitabu cha tozo (tariff books) cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA). Hata hivyo, TPA baada ya kupokea malalamiko ya wadau mbalimbali kuhusu tozo hizo, imeanza kuchukua hatua za kufanya marejeo ya tozo hizo kwa bandari zote ndogo nchini,” amesema.

error: Content is protected !!