Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kesi ya madiwani Ngorongoro: Mahakama yaipa siku 14 Jamhuri
Habari Mchanganyiko

Kesi ya madiwani Ngorongoro: Mahakama yaipa siku 14 Jamhuri

Spread the love

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Arusha, imeuamrisha upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji inayowakabili baadhi ya madiwani wa Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, kukamilisha upelelezi wake ndani ya siku 14, kuanzia leo tarehe 25 Oktoba hadi 8 Novemba, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Amri hiyo imetolewa na mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi, Herieth Mhenga, wakati kesi hiyo ilipokuja kutajwa, baada ya upande wa jamhuri kudai upelelezi wa kesi hiyo Na. 11/2022 haujakamilika.

Hakimu Mhenga alitoa amri hiyo baada ya mawakili utetezi kudai Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), inakiuka sheria na katiba kwa kutokamilisha upelelezi ndani ya siku 90, tangu washtakiwa walipokamatwa na Jeshi na Polisi, katika nyakati tofauti kuanzia tarehe 9 Juni 2022.

Akizungumza baada ya kesi hiyo kuahirishwa hadi Novemba 8, mwaka huu, Wakili wa utetezi, Jebra Kambole, amedai kitendo cha upelelezi kutokamilika kinaathiri haki za washtakiwa, huku akiiomba ofisi ya DPP kukamilisha suala hilo ili wasiokuwa na hatia waachwe huru.

Amedai, baadhi ya washtakiwa waliokamatwa kuanzia Juni, 2022 wameshasota rumande zaidi ya siku 140, huku baadhi yao ambao ni wagonjwa wakikosa huduma za matibabu.

“Washtakiwa wa kwanza walikamatwa tarehe 9 Juni 2022, ukihesabu mpaka leo ni zaidi ya siku 140 wako ndani na maelekezo ya mwendesha mashataka mkuu wa Serikali kwamba upelelezi ukamilike ndani ya siku 90 kwa hiyo upelelezi uko nje ya yale ambayo yameelekezwa lakini pia mara kadhaa tumesikia viongozi wa Serikali kuwa upelelezi ukamilike kwa wakati,” amedai Kambole.

Kesi hiyo ina washtakiwa 25, akiwemo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Ngorongoro, Ndirango Olesenge Laizer. Diwani wa Kata ya Piyaya, Simon Orosokiria. Diwani viti maalum, Kijoolu Kakeya.

Wengine ni, Diwani wa Ololosokwani, Moloimet Yohana. Diwani wa Malambo, Joel Lessonu. Diwani viti maalum, Talengo Leshoko. Diwani wa Oloirien, Shengena Killel. Diwani wa Arash, Mathew Eliakimu na Diwani wa Maaloni, Damiani Laiza.

Washtakiwa hao waliwekwa kizuzini tangu tarehe 16 Juni 2022, wakikabiliwa na mashtaka mawili, la kwanza wanatuhumiwa  kupanga njama ya kuwa maofisa wa Serikali na polisi , watakaoshiriki zoezi la kuweka mipaka katika pori tengefu la Loliondo.

Shtaka la pili ni la mauaji ya askari polisi mwenye namba G 4200, Koplo Garlus Mwita, wanalodaiwa kulitenda tarehe 10 Juni mwaka huu, maeneo ya Ololosokwan, wilayani Ngorongoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza namna Nathwani alivyomjeruhi jirani yake

Spread the loveMSIMAMIZI wa Msikiti wa Wahindi Lohana aitwae, Ankit Dawda (32)...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!