March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya dhamana ya Sudi Brown, Maua Sama, Shaffih kusikilizwa J’tatu

Spread the love

KESI ya maombi ya dhamana Na. 13/2018 ya Msanii wa Bongo Fleva, Maua Sama, Watangazaji Sudi Kadio maarufu kama Soudy Brown na Shaffih Dauda na wengine wanne kuanza kusikilizwa siku ya Jumatatu tarehe 24 Septemba 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Kwa mujibu wa Wakili Jebra Kambole, kesi hiyo dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polsi, Mkurugenzi wa Uplelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) na wengine itasikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Huruma Shahidi.

Maua Sama na Soudy Brown wanashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam tangu Jumapili ya tarehe 16 Septemba mwaka huu, kwa tuhuma za kudhalilisha fedha ya Tanzania.

Wakati Mtangazaji Shafii Dauda, Anthony Luvanda (MC Luvanda), Michael Mlingwa, Fadhili Kondo na Benedict Felix Kadege wakishikiliwa kwa tuhuma za kuendesha mtandao wa Youtube pasipo kusajili katika Mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA).

error: Content is protected !!