May 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kaze, Nizar halfani watimuliwa Yanga

Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga

Spread the love

 

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeamua kuvunja benchi lote la ufundi sambamba na kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha wao Cedric Kaze na msaidizi wake Nizar Halfan. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Taarifa hiyo imekuja muda mchache mara baada ya Yanga kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Polisi Tanzania kwenye mchezo wa Ligi Kuu.

Wengine waliotimuliwa kwenye bechi hilo la ufundi ni kocha wa makipa Vladimir Niyonkuru, kocha wa viungo Edem Mortois pamoja na affisa usalama wa timu hiyo Mussa Mahundi.

Kuvunja kwa bechi hilo la ufundi ni kufuatia matokeo mabaya waliopata kwenye michezo sita ya Ligi Kuu Tanzania Bara toka kuanza kwa mzunguko wa pili.

Katika michezo hiyo sita yanga imefanikiwa kupata ushindi kwenye mchezo mmoja, imepoteza mmoja na kwenda sare mechi nne.

 

error: Content is protected !!