Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Kaya 10,000 kuhama kwa hiari awamu ya pili Ngorongoro
Habari Mchanganyiko

Kaya 10,000 kuhama kwa hiari awamu ya pili Ngorongoro

Spread the love

IMEELEZWA kuwa ujenzi wa nyumba 5,000 utawezesha kaya 10,000 kuhama kwa hiari kutoka Ngorongoro kuelekea katika kata za Msomera, Saunyi (Tanga) na Kitwai iliyopo mkoani Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Nyumba hizo 5,000 za awamu ya pili zinazojengwa na vikosi vya SUMA JKT, kati yake nyumba 2,500 zinajengwa eneo la Msomera, nyumba 1,500 zinajengwa Kitwai  na nyumba 1000 zinajengwa eneo la Saunyi.

Meneja Mahusiano ya Umma wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Hamis Dambaya

Hayo yamebainishwa na Meneja Mahusiano ya Umma wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Hamis Dambaya alipowasilisha mada katika mkutano mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) uliofanyika wiki iliyopita mkoani Lindi.

Alisema awamu ya kwanza zilijengwa nyumba 503 katika kata ya Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga na kuwekwa miundombinu mbalimbali ya kijamii.

“Kwa hiyo katika awamu hiyo ya kwanza tulifanikiwa kuhamisha kaya 551 zenye idadi ya watu 3010 waliohama kwa hiari pamoja na mifugo 15,321,” alisema na kuongza kuwa katika awamu ya pili kaya 4,000 pia zimechagua maeneo mengine wanayotaka kuhamia kwa hiari.

Eneo la Msomera zilipojengwa nyumba 501

Alisema kaya hizo zinazohama kwa hiari zinapewa fidia ya maendeleo ya makazi ndani ya makazi, Sh 10 milioni ambayo ni motisha kwa kila kaya ili ziweze kuwa na pesa ya kujikimu.

“Awamu ya kwanza waliohamia Msomera wamepewa nyumba yenye vyumba vitatu kwenye hekari 2.5 na shamba hekari tano kwa ajili ya kufanya shughuli za ufugaji.

“Wanaohama kwa hiari tunawasarifisha watu na mizigo yao bure. Tunatoa chakula gunia mbili kila baada ya miezi mitatu kwa muda wa miezi 18 lengo uhakikisha katika kipindi chote anaweza kujitegemea lakini pia tunahakikisha kila eneo kuna huduma zote za kijamii,” alisema Dambaya.

Aidha, alitoa wito kwa wahariri kuendelea kuunga mkono mpango huo wa Serikali hasa ikizingatiwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu na mifugo katika hifadhi hiyo na kuhatarisha uhalisia wake.

“Kwanza sababu za kuwahamasisha wananchi kuhama ni kuendelea kuimarisha uhifadhi na kuwaletea maendeleo wananchi tofauti na wanavyoishi hivi sasa Ngorongoro.

“Pia kuna kubwa la watu ambao wameongezeko kutoka watu 8,000 waliokuwepo mwaka 1959 hadi kufikia 125,000 ndani ya hifadhi. Ongezeko la mifugo 261,723- hadi kufikia mifugo 890,459,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile aukwaa uenyekiti wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!