Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Kauli ya DC Kigamboni yakera wanaharakati, wamvaa
Habari Mchanganyiko

Kauli ya DC Kigamboni yakera wanaharakati, wamvaa

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Anna Henga
Spread the love

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), kimetoa wito kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma kuwachukuliwa hatua viongozi wanaokiuka misingi ya utawala bora, sheria pamoja na haki za binadamu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 27 Agosti 2019 kupitia tamko la kituo hicho lililotolewa na Anna Henga, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC baada ya Sara Msafiri, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kutangaza zoezi la kuwaadhibu watu wanaotuhumiwa kwa makosa ya wizi.

Tamko hilo limedai kuwa, hatua  hiyo inachochea raia kujichukulia sheria mkononi kitendo ambacho ni kinyume na kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma.

“Kwa mujibu wa kanuni za maadili ya utendaji katika utumishi wa umma zinasema watumishi wa umma wanapswa kuzifahamu, kuzingatia na kuzifuata ipasavyo sheria, kanuni na taratibu za kazi. Tunaisihi tume itekeleze jukumu lake kwa kuwachukulia hatua stahiki viongozi wanaokiuka misingi ya utwala bora kwa kushindwa kuheshimu haki za binadamu,” linaeleza tamko hilo.

Aidha, kituo hicho kimemtaka Msafiri kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo ili isichochee wananchi kujichukulia sheria mkononi.

“Kwa mujibu wa ripoti ya haki za binadamu kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Juni 2019 vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mkononivimepungua. Kauli hii inaweza kuchochea wananchi kuendelea kujichukulia sheria mkononi na vyombo vya ulinzi na usalama kuvunja haki za raia.

“LHRC kinakemea kauli za aina hii hasa kutoka kwa viongozi wenye dhamana ya kulinda haki za binadamu na kuhakikisha uatawal;a wa sheria unazingatiwa.

“Tunatoa wito kwa kiongozi huyo kurejea kipao chake cha kuilinda katiba na kurekebisha kwa kutoa ufafanuzi wa kauli hiyo ili kusitisha muendelezo wa kujichukulia sheria mkononi,” linaeleza tamko hilo.

Hivi karibuni Msafiri alisema, kwamba wataanza zoezi la kuwakamata na kuwapiga watu wanaotuhumiwa kwa wizi, akidai kwamba wengi wao hukamatwa na kuachiwa kwa dhamana kisha huendelea na tabia hiyo ya wizi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!