Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Katibu Mkuu Uchukuzi awataka watumishi kuwa wabunifu
Habari Mchanganyiko

Katibu Mkuu Uchukuzi awataka watumishi kuwa wabunifu

Spread the love

SERIKALI imetoa wito kwa watumishi wa Taasisi zilizo chini ya Sekta ya Uchukuzi kuongeza ufanisi na ubunifu ili kuongeza tija kazini na kukuza mapato ya Taasisi hizo na Taifa kwa ujumla. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza mjini Kigoma Katibu Mkuu (Sekta ya Uchukuzi), Gabrieli Migire, amesema ukuaji wa biashara mkoani humo unategemea sana miundombinu ya usafiri na uchukuzi hususani bandari na reli na kutoa wito kwa watumishi kuzidisha kasi ya utendaji ili kufikia lengo hilo.

“Mkoa huu una bandari una reli ongezeni kasi ya utendaji kwani kukua kwa pato kwa taasisi za uchukuzi kwanza kutafanya taasisi kununua mitanbo zaidi lakini kupokea na kusafirisha mwingi zaidi na kuonegza pato la taasisi, mkoa na Taifa kwa ujumla”, amesema Katibu Mkuu Migire.

Aidha, amemtaka Mkurungenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Eric Hamiss, kuhakikisha miradi ya bandari inayotekelezwa mkoani humo inakamilika kwa wakati na viwango huku akisisitiza uadilifu katika utekelezaji huo ikiwemo bandari za Ujiji, Kibirizi, Bandari Kavu ya Katosho.

Kwa upande wake Meneja wa Bandari ya Kigoma, Manga Gassaya, amesema kwa sasa Bandari hiyo inauwezo wa kuhudumia tani milioni tatu kwa mwaka na mzigo unaosafirishwa kwa sasa unapelekwa Burundi, DRC -Congo na Rwanda.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Migire amekagua mradi wa ukarabati wa meli ya MT Sangara na kumtaka  Meneja wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) wa mkoa wa huo, kuhakikisha kasi ya ukarabati huo inaongezeka ili kukamilisha mradi huo na kuruhusu usafirishaji wa mafuta kutoka Kigoma na nchi zinazozunguka Mkoa huo.

Naye, Meneja wa kampuni ya MSCL wa mkoa huo, Allen Butembero, amesema ukarabati wa meli ya MT. Sangara unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2022 na itakapokamilika  itakuwa na uwezo wa kubeba mafuta lita 410,000.

Katibu Mkuu Migire yuko mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Sekta ya Uchukuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!