Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kangi amtwisha zigo la Lugumi IGP Sirro
Habari za Siasa

Kangi amtwisha zigo la Lugumi IGP Sirro

Kange Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Picha Ndogo IGP, Simon Sirro
Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Kugola amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro kumtafuta mmiliki wa Kampuni ya Lugumi na kumfikisha ofisini kwake Julai 31, mwaka huu saa 2 asubuhi ili kujua hatma ya suala la mkataba baina ya serikali na kampuni hiyo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Lugola amezungumza hayo leo na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam wakati akitolea ufafanuzi mambo mbalimbali ndani ya Wizara yake.

“Kuhusu suala la Mkataba wa kufunga vifaa vya utambuzi wa alama za vidole yaani ‘Automated Fingerprint Information System baina ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Kampuni ya Lugumi, nimekiagiza Jeshi la Polisi kumleta mmiliki wa kampuni hiyo ofisini kwangu tarehe 31, Julai, 2018 saa mbili kamili asubuhi,” amesema.

Aidha amemtaka IGP kuwasilisha mikakati ya kuimarisha usalama ili watanzania wawe na uhakika wa usalama.

“Hatuwezi kuwa na Jeshi la Polisi na wakati huo huo tunakuwa na majambazi yanayotupangia ratiba, yanayotupangia muda wa kufanya kazi, majambazi yanayotuambia huku msije tutafunga mtaa,” amesema.

Pia amesema kuna baadhi ya askari wanajihusisha na vitendo vya rushwa kubambikizia kesi wananchi hivyo amemuagiza IGP aendelee na hatua kali kwa askari watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Katika hatua nyingine Lugola amezungumzia suala la mbwa wa askari aliyedaiwa kutoonekana katika kikisi cha mbwa Lugola amesema suala hilo linafanyiwa uchunguzi na IGP hivyo upishe uchunguzi upite kwanza.

“Nilipita kwenye kikosi cha farasi na mbwa ambao wanapewa mafunzo kama askari, kwenye vitabu vya makabidhiano nilikuta dosari ya idadi kubadilika siku moja na nyingine, nilitoa maagizo na IGP ameitisha uchunguzi, tuwape nafasi watupe majibu,” amesema Lugola.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!