February 27, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Aliyedaiwa kumpiga risasi Sheikh Ponda ajiuwa kwa risasi

Spread the love

ALIYEDAIWA kuhusika na tukio la kumshambulia kwa risasi Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam, Sheikh Issa Ponda, Benedict Nyamagatara ametajwa kufariki dunia kwa kujipiga risasi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Sheikh Ponda alishambuliwa kwa risasi ya bega Agosti 10, 2013 akiwa kwenye mkutano wa hadhara Morogoro.

Mwandishi wa Habari hizi amezungumza na Sheikh Ponda leo kwa njia ya simu amesema kuwa baada ya kushambuliwa kwa risasi aliambiwa na wenyeji wa eneo lile kuwa askari aliyefahamika kwa jina la Benedict alitajwa kuhusika na shambulio hilo.

“Wananchi wa maeneo hayo walikwenda kwenye tume ya haki za binadamu kutoa ushahidi juu kuonekana kwa Afande Benedict kwenye eneo la tukio na nama alivyohusika,” amesema Sheikh Ponda.

Hata jeshi la Polisi lilikiri kuwa risasi ile ilifyetuliwa na askari wao ingawa baadaye walisema kuwa risasi ilirushwa juu na hatimaye kukanusha,” amesema Ponda.

Imeripotiwa kuwa Julai 12 ,2018 Afande Nyamagatara amefariki dunia kwa kujifyetulia risasi ya taya na kutokea kichwani.

error: Content is protected !!