Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Kamati yaomba miradi ya maendeleo iliyozuiwa kurudishwa Ngorongoro
Habari Mchanganyiko

Kamati yaomba miradi ya maendeleo iliyozuiwa kurudishwa Ngorongoro

Spread the love

KAMATI ya kukusanya mapendekezo ya wananchi na wadau juu ya kumaliza mgogoro wa ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha, imeiomba Serikali irudishe miradi ya maendeleo na huduma za kijamii, zilizozuiliwa kwenda wilayani humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Ombi hilo limetolewa leo Jumatatu, tarehe 25 Aprili 2022, mkoani Arusha, katika kikao cha siku mbili cha kamati hiyo, cha ukamilishaji mchakato wa ukusanyaji maoni na mapendekezo, ambayo yatawasilishwa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wiki hii.

“Serikali irudishe miradi yote ya maendeleo na huduma za jamii zilizozuiliwa kwenda Tarafa ya Ngorongoro,” imesema taarifa ya kamati hiyo.

Wito huo umetolewa ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ngorongoro, Dk. Jumaa Mhina, kuwaagiza wakuu wa Shule za Msingi nne wilayani humo, kuhamisha kiasi cha Sh. 160 milioni, zilizopelekwa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, katika Wilaya ya Handeni.

Aidha, kamati hiyo imeiomba Serikali isitishe mipango yote inayoendelea kuhusu mgogoro huo unaodaiwa kuibuka kufuatia ongezeko la idadi ya watu kwenye Hifadhi ya Ngorongoro, hadi pale maoni ya wananchi watakapofanyiwa kazi.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo, mchakato wa uchukuaji maoni na mapendekezo ya utatuzi wa mgogoro huo, umekamilika.

“Mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi kwa vijjji vyote vinavyozunguka eneo lenye mgogoro wa kilometa za mraba 1500 na eneo la mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, umekamilika kama tulivyoeleza awali na taarifa ya maoni hayo inatarajiwa kuwasilishwa kwa Waziri Majaliwa, pamoja na viongozi wa juu wa Serikali pamoja na umma,” imesema taarifa hiyo.

Kamati hiyo yenye wajumbe kutoka makundi mbalimbali, inajumuisha watu 60 kutoka kata za Loliondo, Sale na Ngorongoro.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!