Spread the love

 

FRED ambaye Mkazi wa Ruvuma amejishindia Sh 50Mil kutoka Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya BetPawa baada ya kupatia idadi ya mipira 109 iliyokuwepo katika gari maalum iliyokuwepo ndani. Anaripoti¬†Mwandishi Wetu…(endelea)

Ewala juzi Jumamosi mchana alitangazwa kuwa mshidi wa mamilioni hayo na kukabidhi mfano wa hundi katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Hekima Garden, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Ofisa Masoko wa BetPawa, Job Ngaula alisema kuwa katika shindano hilo walipatikana washindi wawili ambao ni Idd  na Ewala mwenyewe.

Ngaula alisema kuwa washindi hao walitakiwa wagawane Sh 25 Mil kila mmoja kabla ya Ewala kukabidhiwa 50Mil zote.

Aliongeza kuwa Ewala alikabidhiwa fedha zote baada ya mshindi mwenzake Idd kushindwa kutokea katika hafla hiyo ya kumtangaza mshindi wa shindano, licha ya kupewa taarifa.

“Sharti la kwanza tuliloliweka katika shindano hili ni kufika katika siku husika ya kumtangaza mshindi wa pesa hizi.

“Hiyo ndiyo sababu ya kuwapigia simu washindi kumi waliokaribia katika utabiri wao wa mipira ambayo ilikuwa ndani ya gari maalum ambalo lilikuwa linazunguka katika baadhi ya mikoa hapa nchini.

Washiriki waliotoka mikoa mbalimbali wakifuatilia hafla ya utoaji zawadi kwa mshindi wa kwanza, mara baada ya kubashiri kwenye droo iliyoendeshwa na betPawa

“Hivyo Ewala alikuwepo ambaye alitabiri sawa kuwepo mipira 109 ndani ya gari hilo maalum sawa na Idd ambaye yeye hakutokea kabisa, hiyo ndiyo sababu ya kumpatia fedha zote Sh 50Mil lakini kama wangekuwepo washindi wote, basi wangegawana Sh 25 kila mmoja,” alisema Ngaula.

Aidha Ngaula alisema kuwa shindano hilo lilikwenda sambamba na zoezi la kugawa jezi kwa timu 28 kwa kila moja ikichukua jezi 18.

Kwa upande wa mshindi Ewala yeye alisema kuwa “Nafurahia kushinda pesa hizi ambazo kitu cha kwanza nitakachokifanya kujadiliana na mke wangu.

“Baada ya hapo tutajua nini tufanye, lakini ninaamini kitu cha kwanza lazima atataka tujenge nyumba na mimi nahitaji nyumba, hivyo tutajenga, niwashauri Watanzania wabashiri na BetPawa, kwani washindani wanapatikana kwa haki kabisa,” alisema Ewala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *