Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati ya siasa yakagua miradi ya bilioni 9.3 Ileje, yabaini madudu
Habari za Siasa

Kamati ya siasa yakagua miradi ya bilioni 9.3 Ileje, yabaini madudu

Spread the love

KAMATI YA siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Songwe  imekagua miradi nane yenye thamani ya Sh 9.3 bilioni katika wilaya ya Ileje huku ikitaja kasoro zikizopo kwa baadhi ya miradi na kutaka waliohusika kujitathimini. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Miongoni mwa miradi hiyo ni ujenzi shule ya wasichana inayojengwa kwa Sh 470 milioni, Shule ya msingi Ikumbilo inayojengwa kwa Sh 347.5 milioni, ujenzi mradi wa maji unaogharimu Sh 1.1 bilioni, ujenzi mradi wa umeme (Sh 96 milioni),majengo matatu ya hospitali ya wilaya (Sh 541 milioni).

Akizungumza leo tarehe 23 Juni 2023 wilayani humo, Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa, Ladwel Mwampashi amesema ujenzi wa miradi hiyo ipo vizuri na ameipokea huku akishauri kasoro zilizoonekana kwenye baadhi miradi hasa kwenye hospitali ya wilaya zirekebishwe ili katika ukaguzi ujao asizione kasoro hizo.

Amesema wilaya ya Ileje ndiko anakotoka anafahamu wazi kuwa viongozi wa halmashauri hiyo walikuwa na kasoro kwenye uongozi wao.

Mjumbe wa kamati kuu CCM Taifa Mkoa, Aden Mwakyonde amesema kuna kila sababu watumishi Ileje kuwa na ushirikiano ili fedha zinazotolewa na Serikali kwenye miradi ya maendeleo zitumike vyema “tumekagua miradi ya bilioni 9.3 leo palipo na kasoro rekebisheni kuhepuka upigaji fedha”.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za Siasa

Serikali yasaka bilioni 3 kujenga daraja Mto Mpiji

Spread the loveSerikali imesema inaendelea na juhudi za kutafuta fedha kiasi cha...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

error: Content is protected !!