July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kamati aliyounda Rais Samia yashauri chanjo corona itolewe, takwimu ziwe wazi

Spread the love

 

KAMATI Maalum ya kufanya tahimini ya maambukizi ya ugonjwa wa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) nchini Tanzania, imependekeza Serikali ya nchi hiyo, itoe takwimu za mwenendo wa ugonjwa huo pamoja na chanjo. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Ni kamati iliyoundwa hivi karibuni na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kufanya tathimini ya ugonjwa huo kisha kumshauri namna ya kufanya ili kukabili maambukizi ya ugonjwa huo.

Taarifa ya kamati hiyo, iliyoongozwa na Mwenyekiti, Prof. Said Aboud, kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili, ambaye alianza kwa kumkabidhi Rais Samia, Ikulu ya Dar es Salaam kisha kuzungumza na waandishi wa habari.

“Kamati ianshauri, Serikali itoe takwimu sahihi za ugonjwa kwa umma na Shirika la Afya Duniani (WHO), ili wananchi wapate taarifa sahihi kutoka serikali na iheshimu makubaliano ambayo nchi imeridhia,” amesema Prof. Aboud.

Kuhusu matumizi ya chanjo, kamati hiyo imependekeza chanjo zilizoanishwa na WHO zitumike, kwa kuwa utafiti wake umebaini kuwa ni salama.

“Kuhushu chanjo dhidi ya COVID-19, kamati inashauri serikali kwa kutumia vyombo vyake iendelee na hatua kuelekea kuruhusu matumizi huru ya chanjo kuhusu ugonjwa huo kwa kutumia chanjo iliyoorodheshwa na WHO kwa ajili ya kuimarisha kinga,” amesema Propf. Aboud.

Mwenyekiti wa kamati hiyo amesema “kwa kuwa kupitia uchambuzi wa kamati, chanjo hizo zina ufanisi na usalama unaokubalika kisayansi.”

Kamati hiyo imependekeza chanjo hiyo itolewe kwa watu waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo, wazee na watu wenye magonjwa hatarishi.

“Ianze kutolewa kwa wahudumu wa vituo vya kutolea afya na wahudumu waliomstari wa mbele kutoa huduma, utalii, hoteli, mipakani, viongozi wa dini wazee kuanzia miaka 50, watu wazima wenye maradhi sugu, mfano kisukari na mifumo ya upumuaji,” amesema Prof. Aboud

Pia, Kamati hiyo, imependekeza Serikali ifanye haraka katika kukamilisha muongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa huo.

“Wizara ikamilishe muongozo mpya wa matibabu ya Covid-19, iendelee kuhakikisha matumizi ya tiba asili na mbadala katika mfumo rasmi wa tiba ya kisasa yanazingatia misingi ya kisayansi. Iendele kutoa fursa kuwezesha wanasayansi kufanya tafiti kwa mujibu wa taratibu, kinga na matibabu ya COVID-19,” amesema Prof. Aboud.

Prof. Aboud amesema, kamati hiyo imebaini kwamba Tanzania iko hatarini kukumbwa na wimbi la tatu la COVID-19, na kuishauri Serikali iimarishe kasi katika udhibiti wa virusi hivyo.

“Tanzania imekumbwa na mawimbi mawili makubwa na hivi sasa kutokana na mwenendo wa ugonjwa huo katika mataifa mengine duniani, kuna tishio la kutokea wimbi la tatu hapa nchini, hata hivyo kamati imebaini kuwa mwamko wa kudhibiti wimbi la kwanza ulikuwa mkubwa kulinganisha na wimbi la pili,” amesema Prof. Aboud.

Prof. Aboud amesema “kamati imeshuari kuimarisha kasi kudhibiti tishio la wimbi la tatu, baada ya uchambuzi wa kina, kamati imependekeza yafuatayo, serikali ihuishe mipango ya dharula katika ngazi zote katika kukabiliana na majanga ikiwemo COVID- 19.”

error: Content is protected !!