Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kairuki aonya maofisa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi hewa
Habari Mchanganyiko

Kairuki aonya maofisa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi hewa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki
Spread the love

 

SERIKALI imewataka Maafisa Maendeleo nchini kuacha kutumia vyeo vyao kwa kuweka taarifa hewa za vikundi vya mikopo ya asilimia 10 kwa lengo la kujinufaisha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini, uliofanyika Jijini Dodoma, kuanzia tarehe 8 hadi 10 Novemba, 2022.

Kairuki amewaonya vikali Maafisa hao wanaotumia vibaya vyeo vyao wajilekebishe mara moja vinginevyo watakutana na mkono wa Dola kwa mujibu wa Sheria zilizowekwa.

“Naomba kama wapo ambao huko nyuma kabla ya leo tarehe 10, walikuwa na makandokando hayo tubadilike, ni tamaa ambazo hazina baraka na ni wizi wa kuwaibia walipa kodi na wanasononeka, machozi yao hata siku moja hayatakufikisha sehemu salama” amesema Kairuki.

Waziri Kairuki amesema hatarajii kuona kesi baada ya tarehe ya leo, wala kusikia kesi za Manispaa mbalimbali kama vile Manispaa ya Ilala, Kinondoni na Kalambo kuanza kupokea kesi wakati maelekezo yalikwishatolewa na Katibu Mkuu wakati wa kikao kazi.

Aidha, amezitaka Halmashauri nchini kuendelea kutumia Mfumo wa kieletroniki wa mapato ya Asilimia 10 ili kuhakikisha kuwa Mikopo yote iliyotolewa na inayoendelea kutolewa inaratibiwa, kukusanywa kama madeni na kurejeshwa kwa wakati ili wengine wanufaike na mikopo hiyo.

“naomba nisisitize fedha hizi ni mikopo inayotakiwa kurejeshwa na kuweza kuwakopesha wahitaji wengine, Halmashauri zote zihakikishe zinaweka Mikakati ya kukusanya madeni hayo na ifikapo mwezi Februari, 2023 nusu ya madeni hayo ambayo yamepitwa na muda yawe yamerejeshwa na hatua sitahiki ziwe zimechukuliwa kulingana na Kanuni zilizopo” amesema Kairuki.

Akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Makundi Maalum Dk. Zainab Chaula amewaasa Maafisa hao kufanya kazi kwa moyo, juhudi ni maarifa lakini pia kutimiza wajibu wao kwenye maeneo yao ya kazi.

Naye Felix Sule mshiriki na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Karatu amesema kikao kazi hicho kimemjengea uwezo kwa kujua wajibu na majukumu yao katika kuratibu na kusimamia shughuli za wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) na maboresho ya Mfumo wa taarifa mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!