May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

JPM: Sitaki kisingizio cha corona

Spread the love

 

RAIS John Magufuli ametaka miradi mbalimbali nchini kukamilika kwa wakati, na kwamba hataki kusikia imesimama kwa sababu ya corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Amesema, miradi ya barabara ya njia nane kutoka Dar es Salaam kwenda Kibaha inaendelea kujengwa, Daraja la Kijazi (Ubunge) limejengwa na mingine haijasimama, hivyo amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaokagua miradi, wasisikilize kwamba imeshindwa kukamilika kutokana na corona.

“… hatutaki visingizio, niwatake watendaji wangu pasiwe na kisingizio chochote cha ugonjwa wa corona wanapokagua miradi,” ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Februari 2021 katika uzinduzi wa Daraja la Juu la Kijazi, Ubungo jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia ujenzi wa daraja hilo, amewashukuru wakandarasi kwa kumaliza mradi huo kwa wakati, na kwamba wakandarasi wengine nao wamalize kazi kwa wakati.

“Nitoe wito kwa makandarasi wengine nchi nzima, wasitafute visingizio vya kuchelewa kazi, mara corona mara sijui nini. Hawa wamemaliza na corona ilikuwepo na daraja limekamilika.

“Mara wataalamu wetu wapo nje, vifaa haviingii kwa sababu ya corona, ni wizi unaofanywa na makandarasi na ndiyo maana mnaona daraja hili limekamilika na corona ipo,” amesema.

error: Content is protected !!