April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Joto Zitto kukamatwa lapanda

Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalando

Spread the love
HATUA ya Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo kudai kuundiwa zengwe la kuhusishwa na utakatishaji fedha, limekishtua chama hicho. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam…(endelea).

Tarehe 7 Februari 2020, akiwa Marekani, Zitto aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter, kwamba anaundiwa mashitaka ya utakatishaji fedha, na kwamba atakaporejea anatakiwa kukamatwa.

“Mpango wa kunishitaki kwa kosa la utakatishaji fedha pindi nitakapotua Dar es Salaam kutoka safari zangu za kimataifa, bado unaendelea,” aliandika Zitto.

Taarifa walizonazo wazee wa chama hicho, zinawatia hofu juu ya mkakati huo ambayo tayari umeelezwa na Zitto mwenyeye ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini.

Leo mbele ya waandishi wa habari, wazee wa cama hicho wakiongozwa na mwenyekiti wao Yassin Mohamed, wamesema mpango huo unalenga kuchochea uovu nchini.

Wameeleza kwamba, Zitto amekuwa akisakamwa ndani naje ya Bunge kutokana na misimamo yake kwa maslahi ya taifa, akitoa mfano wa kuandika barua kwenye Benki ya Dunia (WB), kushinikiza kutotoa fedha za elimu mpaka serikali itakaporuhusu wanafunzi wataopewa mimba, kurejea masomoni.

“Hoja ambayo wanaegemea kuhalalisha matamko hayo ni madai, kwamba Zitto ameisaliti nchi kwa hatua yake ya kuiandikia barua Benki ya Dunia akiomba isitishe mkopo wa elimu nchini, mpaka pale serikali itakapobadili sera yake ya kibaguzi juu ya elimu kwa wanafunzi wa kike, wanaopata mimba wangali shuleni,” amesema Mzee Mohamed.

Mzee Mohamed amesema, hilo haliwezi kukubalika katika nchi ambayo inaheshimu demokrasia na siasa za ushindani.

error: Content is protected !!