April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mch. Msigwa: Nakubalika

Mch. Peter Msigwa

Spread the love

MCHUNGAJI Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini, amesema kila baada ya miezi mitatu, hufanya utafiti kubaini idadi ya wananchi wanaomuunga mkono jimboni humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Mchungaji Msigwa ametoa kauli hiyo alipokuwa kwenye mahojiano na Kituo cha Redio cha East Africa.

Amesema, matokeo ya utafiti anaoufanya yamebaini kwamba kati ya wananchi 10 jimboni humo, saba wanamuunga mkono, wawili wanaunga mkono Chama cha Mapinduzi (CCM), na mmoja hana uamuzi juu ya suala hilo.

Mchungaji Msigwa amesema kufuatia matokeo ya utafiti huo, atagombea tena katika jimbo hilo, kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba 2020.

“Nagombea,  wananchi wananihitaji bado. Nimekwua na tabia ya kufanya utafiti kila baada ya miezi mitatu . Katika utafiti niliofanya kati ya watu kumi, saba wananiunga mkono, wawili wanaiunga mkono CCM na mmoja hana uamuzi,” amesema Msigwa .

error: Content is protected !!