May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jeshi la wachezaji 30 kutua Equtorial Guinea

Kim Poulsen Kocha wa Taifa Stars

Spread the love

 

KOCHA Kim Poulsen ameweka wazi jeshi la wachezaji 30 litakalosafiri kutoka Nairobi nchini Kenya ambapo timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kwenda Equtorial Guinea kwa ajili ya mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa Afrika (AFCON). Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea)

Mchezo huo wa Kundi J, utapigwa kesho tarehe 25 Machi, 2021 kwenye dimba la Malabo nchini humo, utakaochezwa saa 2 usiku kwa muda wa Afrika ya Kati na saa 4 usiku kwa muda wa Afrika Mashariki.

Kikosi hiko kitaondoka leo jijini Nairobi kwa ndege ya kukodi ambapo mara baada ya mchezo huo timu itageuka kurudi Tanzania kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa mwisho dhidi ya Libya utakaopigwa tarehe 30 Machi 2021, kwenye Uwanja wa Mkapa.

Mpaka sasa Stars inashika nafasi ya tatu kwenye kundi hilo ikiwa na pointi nne, nyuma ya pointi mbili na Equtorial Guinea ambao wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi sita, huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Tunisia wenye pointi 10 na Libya ikibuluza mkia kwa pointi tatu.

Mchezo huo wa kesho utakuwa wa kwanza toka Poulsen alipochukua kijiti kutoka kwa Ettiene Ndayilagije mara baada ya kutimuliwa Februari 2021.

error: Content is protected !!