Sunday , 26 March 2023
Home Gazeti Habari Mwili wa Magufuli wapokea kishujaa Mwanza
HabariTangulizi

Mwili wa Magufuli wapokea kishujaa Mwanza

Spread the love

 

NYUMBANI ni nyumbani. Hivi ndivyo unaweza kuelezea, jinsi wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wameupokea kishujaa mwili wa Dk. John Pombe Joseph Magufuli. Anaripoti Mwandishi Wetu…

Mwili wa Dk. Magufuli, umewasili asubuhi ya leo Jumatano, tarehe 24 Machi 2021, katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza ukitokea visiwani Zanzibar.

Dk. Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tanzania, anatokea kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza, hivyo wananchi wamejitokea kumlaki mzawa mwenzao, aliyefariki dunia tarehe 17 Machi 2021, katika Hospitali Mzena, Dar es Salaam.

Msafara huo, ulisimama eneo la Nyamanoro kwa dakika moja ambako kulikuwa na nyumba aliyowahi kuishi mwaka 2007 akiwa waziri wa ujenzi kutoa heshima za mwisho, kisha msafara ukaendelea.

Umati mkubwa wa wananchi, wamejipanga barabarani kutoka Uwanja wa Ndege hadi CCM Kirumba na wengine wakitoka na msafara Uwanja wa Ndege hadi uwanjani, takribani kilomita nane, wakiusindikiza msafara wenye mwili wa Dk. Magufuli.

Msafara huo, uliingia Uwanja wa CCM Kirumba saa 3:17 asubuhi huku uwanja huo ukiwa tayari umejaa na waombolezaji, waliokuwa nje ni wengi zaidi ya waliokuwa ndani.

Mmoja wa wakazi wa Mwanza, Charles Andrew anasema “tumekuja kumpokea mtoto wetu, alikwenda kufanya kazi iliyotukuka, lazima tumpokee kwa heshima kubwa kwani mtoto kwao.”

Mara baada ya msafara huo kuingiwa uwanjani, vilio vilizizima pindi walipoona gari lililombeba mpendwa wao akiingia akiwa amelala mauti.

Itakumbukwa, wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana, Mwanza ndiyo mkoa ulioweka rekodi ya kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wake wa kampeni, kuliko eneo lolote lile kwa kuuja uwanja wa CCM Kirumba na wengine wakiwa nje.

Viongozi mbalimbali wamejitokeza uwanjani hapo akiwemo Waziri Mkuu, Kassima Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.

Mara baada ya wakazi wa Mwanza na maeneo jirani kuuaga leo Jumatano, mwili huo utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

Utasafiri kwa barabara ukipitia Misungwi- Sengerema- Geita- Katoro- Bwanga hadi Chato na kesho Alhamisi, wakazi wa Chato na maeneo jirani watauama mwili wa mpendwa wao na Ijumaa ya tarehe 26 Machi 2021, mwili huo utazikwa kwao Chato.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari

Ugonjwa wa ajabu ulioua watano Bukoka ni Marburg

Spread the loveWAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa ajabu uliosababisha...

AfyaHabariHabari

Ugonjwa wa ajabu wadaiwa kuua watano Kagera, Serikali yatoa tahadhari

Spread the loveJUMLA ya watu watano wanaidaiwa kufariki dunia  katika vijiji vya...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia ampandisha cheo RPC wa Dar

Spread the loveMKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amesema...

error: Content is protected !!