Thursday , 30 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Rais Mwinyi: Tumempoteza mtetezi wa wanyonge
Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Mwinyi: Tumempoteza mtetezi wa wanyonge

Spread the love

 

RAIS wa Zanzibar na Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi amesema, Bara la Afrika limepoteza kiongozi mwanamapinduzi, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli (61). Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Kiongozi huyo wa Zanzibar, amesema hayo leo Jumanne tarehe 23 Machi 2021, katika shughuli ya kuuaga mwili wa Hayati Magufuli, katika Uwanja wa Amani visiwani humo.

“Kwa hakika tumempoteza mwanamapinduzi mahiri wa karne ya sasa, alikuwa kiongozi mwenye uwezo na kipaji cha aina yake. Kiongozi kama yeye ni nadra kupatikana,” amesema Rais Mwinyi.

Rais Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi 2021, kwenye Hospitali ya Mzena, Makumbusho mkoani Dar es Salaam, alikokuwa anapatiwa matibabu ya maradhi ya moyo.

Akimzungumzia Hayati Magufuli, Rais Mwinyi amesema, enzi za uhai wake kiongozi huyo alijipambanua kwa vitendo kuwa yeye ni mzalendo, mtetezi wa wanyonge na mwenye maono makubwa kuhakikisha Tanzania inapiga hatua kimaendeleo.

“Alikuwa mtetezi wa wanyonge, mwenye kujivunia na kuona ufahari Utanzania na Uafrika wake, alikuwa na maono makubwa kuhakikisha nchi yetu inapiga hatua kubwa zaidi ya maendeleo kwa kutumia raslimali tulizobarikiwa na Mungu,” amesema Rais Mwinyi.

Amesema, Hayati Magufuli atakumbukwa kwa namna alivyosimamia matumizi bora ya rasilimali za Tanzania pamoja na kuimarisha Muunganyo wa Tanganyika na Zanzibar.

“Bila shaka tutamkumbuka kwa jinsi alivyojipambanua katika kupigania haki za wanyonge na matumizi bora ya rasilimali za Tanzania kwa masilahi ya Watanzania.”

“Tutakumbuka jinsi alivyojidhatiti kuimarisha Muungano wa Tanzania na kuyaenzi mapinduzi ya Zanzibar,” amesema Rais Mwinyi.

Akielezea mafanikio ya uongozi wa Hayati Magufuli, Rais Mwinyi amesema, alifanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika kipindi kifupi tangu alipoingia madarakani, tarehe 5 Novemba 2015.

Rais Mwinyi amesema, Hayati Magufuli alifanikiwa katika mapambano dhidi ya rushwa na uzembe kwa watumishi wa umma.

“Tutakumbuka uongozi wake katika vita dhidi ya rushwa, ufisadi, ubadhirifu na uzembe, ambapo alipata mafanikio makubwa katika kujenga uadilifu katika jamii na uwajibikaji katika utumishi wa umma,” amesema Rais Mwinyi.

“Ametuaga akiiacha nchi yetu ikiwa katika hali ya amani na utulivu wa kupigiwa mfano Afrika. Yako mengi ya kujifunza kinadharia na vitendo aliyoyaacha. Rais Magufuli alikuwa ni hidaya tuliyopewa na Mungu, ni vyema kuyaenzi aliyofanya kwa bidi,” amesema.

Kiongozi huyo alifikwa na umauti katika muhula wake wa mwisho wa uongozi, alioutumikia kwa kipindi cha miezi minne, tangu alipoapishwa tarehe 5 Novemba 2020 kuwa Rais wa Tanzania.

Baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana akiipeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisaidiana na Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa mgombea wake mwenza (mgombea makamu wa urais).

Baada ya Rais Magufuli kufariki dunia, Samia aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania, akichukua mikoba yake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB Bonge la Mpango – ‘Moto Uleule’ yazinduliwa, Milioni 180…

Spread the loveMSIMU wa tatu wa Kampeni ya kuhamasisha utamaduni wa Kuweka...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awataka wahariri kufanya kazi bila uoga, upendeleo

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan amewataka wahariri wa vyombo...

Habari Mchanganyiko

STAMICO yasaini mkataba wa bilioni 55.2 kuchoronga miamba GGML

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limezidi kufanya vizuri katika...

Habari Mchanganyiko

NMB yatoa traksuti za Mwenge wa Uhuru Mtwara

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa traksuti kwa mkoa wa Mtwara ambako...

error: Content is protected !!