Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Jaji Warioba: JPM kugombea pekee, kuna sharti
Habari za SiasaTangulizi

Jaji Warioba: JPM kugombea pekee, kuna sharti

Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba
Spread the love

JAJI Mstaafu Joseph Warioba, amsema ni utamaduni kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuruhusu rais aliyepo madarakani kutetea kiti chake iwapo hajakiangusha chama. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Amesema, kama kinaona rais aliyeko madarakani anafaa kuendelea tena, hakuna sababu kwa wanachama wengine kujitokeza kugombea akisisitiza ‘iwapo chama kama kinaona anafaa.’

Akizungumza na Mwanahalisi Online leo tarehe 23 Juni 2020, kuhusu mchakato kwa makada wa chama hicho kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa ili kupitishwa na kisha kugombea urais Bara na visiwani Zanzibar amesema, utaratibu huo upo kwenye mataifa mengine.

“Huu ni utaratibu kwa dunia nzima kama rais aliyeko madarakani anataka kugombea tena, na Katiba ina mruhusu na chama kinaona anafaa kugombea tena, anapitishwa. Haina ulazima wa watu wengine kujitokeza tena kugombea wakati mtu yupo.

“Hata nchini Marekani wanafanya hivyo, chama kilichoko madarakani hakuna mtu mwingine aliyejitokeza kuchukua fomu, kwa sababu mgombea wao ni rais aliyeko madarakani (Rais Donald Trump) ambaye anamalizia

Akizungumzia mchakato huo unaoendelea visiwani Zanzibar, Jaji Warioba amesema, makada wengi wa chama hicho wanajitokeza kutokana na rais aliyepo madarakani, Dk. Mohammed Shein anamaliza muda wake.

Zaidi ya makada 23 wamejitokeza visiwani humo, kuchukua fomu kwa ajili ya kuomba kuteuliwa na chama hicho kugombea urais.

Waliojitokeza ni pamoja na Balozi Ali Abeid Karume, Mtoto wa Rais Mstaafu Hayati Abeid Karume. Dk. Hussein Mwinyi, Waziri wa Ulinzi na mtoto wa Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi. Jecha Salum Jecha, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kwa upande wa mawaziri waliojitokeza ni Mhandisi Makame Mbarawa, Waziri wa Maji. Mhandisi Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Shamsi Vuai Nahodha, Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar.

Hata hivyo, Jaji Warioba amesema, visiwani Zanzibar hakutakuwa na upendeleo katika uteuzi, kwa kuwa CCM ina taratibu zake ambazo zitafuatwa ili kuufanya mchakato huo kuwa wa haki na huru.

“Kujitokeza watu wengi ambao ni viongozi au walikuwa watoto wa viongozi, sio mara ya kwanza kutokea, na si kosa kwasababu wana haki ya kugombea kama wanachama halali. Na chama kina taratibu zake ambazo zitafuatwa na hakutakuwa na upendeleo, mwenye sifa atapitishwa,” amesema Jaji Warioba.

Licha ya vigogo hao, Mwatum Mussa Sultani, amekuwa mwanamke wa pekee hadi sasa kuchukua fomu hiyo.

Kufuatia mwitikio mdogo kwa wanawake kujitosa kwenye zoezi hilo, Jaji Warioba amewataka wanawake wajitokeze kwa wingi katika kinyang’anyiro hicho.

Zoezi la uchukuaji na urejeshaji fomu, linaenda sambamba na utafutaji wadhamini 250 kwa kila mtia nia.

Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tanzania akichukua fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi ya CCM, baada ya zoezi hilo kumalizika, tukio litakalofuata ni uchujaji wa wagombea, zoezi litakaloanza tarehe 6 hadi 12 Julai mwaka huu.

Kikao cha kwanza cha uchujaji  kitakuwa ni cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kitakachofanyika tarehe 6 na 7 Julai 2020, kikifuatiwa na kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili, kitakachofanyika tarehe 8 Julai mwaka huu.

Tarehe 9 Julai 2020, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, itaketi kwa ajili ya kutoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, juu ya majina ya wanachama wasizidi watano, wanaoomba kugombea nafasi hiyo.

Kisha tarehe 10 Julai 2020, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM itapendekeza kwa Mkutano Mkuu wa chama hicho, majina matatu ya wanachama wanaoomba kugombea urais wa Tanzania.

Zoezi hilo litakamilishwa na Mkutano Mkuu wa CCM utakaofanyika tarehe 11 na 12 Julai mwaka huu, ambao utachagua jina moja la mgombea urais wa Tanzania. Uchukuaji fomu kupanda kwa upande wa Zanzibar utahitimishwa tarehe 30 Juni 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!