August 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Jaji aliyejiuzulu afariki

Jaji Mohamed Chande Othman akimpa mkono wa pole aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Jaji Upendo H. Msuya enzi za uhai wake alipofiwa na mwanaye

Spread the love

ALIYEKUWA  Jaji wa Mahakama Kuu, Upendo Msuya, amefariki dunia  leo Julai 19 katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu, anaandika Hamisi Mguta.

Taarifa za awali kutoka ndani ya familia zinaeleza kwamba marehemu amefariki kwa ugonjwa wa kiharusi na kwamba alikuwa amepelekwa hospitali na kurudishwa nyumbani kwa zaidi ya miezi mitatu.

Mei 15 Marehemu Upendo aliacha rasmi kazi ya ujaji baada ya rais Magufuli kuridhia ombi lake hilo ambapo ombi hilo lilikubaliwa pamoja na Aloysius Mujulizi, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania na Meck Sadick, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Ikumbukwe kuwa kifo kimemfika Upendo ikiwa ni miezi miwili tangu aache kazi ya ujaji.
Tutaendelea kukujulisha zaidi kuhusu utaratibu wa mazishi

error: Content is protected !!