Tuesday , 18 June 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Makamu wa rais Afghanistan azuiwa kurudi nchini
Kimataifa

Makamu wa rais Afghanistan azuiwa kurudi nchini

Jenerali Abdul Rashid Dostum
Spread the love

MAKAMU wa rais wa Afghanistan, Jenerali, Abdul Dostum amezuiwa kuingia nchini mwake akitokea nchini Uturuki, anaandika Mwaandishi wetu.

Ndege ya kiongozi huyo iliyojaribu kutua nchini humo ikitokea Uturuki imezuiwa.

Dostum alijaribu kurudi nchini humo baada ya kusafiri kuelekea Uturuki mnamo mwezi Mei huku kukiwa na madai kwamba aliwaagiza watu wake kumteka, kumpiga na hata kumbaka mpinzani wake wa kisiasa.

Hata hivyo, amekana kufanya makosa yoyote na kuwa alielekea nchini humo kwa ukaguzi wa afya yake.Haijulikani ni nani aliyekataza kutua kwa ndege hiyo lakini taarifa za karibu na rais Ashraf Ghani ziliiambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), kwamba kurudi kwake hakukupangwa na serikali.

Zaidi ya watu 1000 waliandamana wakiongozwa na Atta Mohammad Noor , ambaye ni Gavana wa Kaskazini mwa mkoa wa Balkh kwa ajili ya kumpokea mpiganaji huyo wa zamani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mashahidi wanasema kuwa baadhi ya wafuasi wa Dostum walikuwa na mabango yaliyosema ‘karibu nyumbani kiongozi wetu,’.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Ramaphosa achaguliwa tena kuwa rais Afrika Kusini

Spread the loveRais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa na wabunge wa...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

DA, ANC waridhia kuunda serikali ya mseto Afrika Kusini

Spread the loveChama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress, ANC,...

Habari za SiasaKimataifa

IFP wakubali kuungana na ANC kuunda serikali

Spread the loveChama cha upinzani nchini Afrika Kusini, Inkatha Freedom Party (IFP)...

KimataifaTangulizi

Boti yazama DRC, 80 wafariki dunia

Spread the loveJUMLA ya watu 80 wameripotiwa kufariki dunia huko nchini Congo...

error: Content is protected !!