Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa IGP Wambura acharuka, asema kuna watu wanataka kuiangusha Serikali, “wasitikise kiberiti”
Habari za SiasaTangulizi

IGP Wambura acharuka, asema kuna watu wanataka kuiangusha Serikali, “wasitikise kiberiti”

IGP Camillius Wambura
Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura amesema kuna kundi la watu ambao wamepanga kuandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – awamu ya sita kabla ya mwaka 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema watu hao ambao wamefanya kosa la uhaini, wanahusisha maandamano hayo na kushawishi watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za kuhusu mkataba wa uwekezaji katika bandari ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Agosti 2023 jijini Dar es salaam, IGP Wambura amesema aliamini hoja za bandari hujibiwa kwa hoja.

Pia amesema aliamini kwa vile baadhi ya watu hao walienda mahakamani wangeheshimu mahakama lakini badala yake wametoka na kuanza kutafuta ushawishi na kuchochea kuwataka watanzania waingie kwenye maandamano ya nchi nzima.

Wakili Mwabukusi

“Lakini mmoja amekwenda mbali zaidi na kusema watahakikisha wanangusha serikali ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kabla ya mwaka 2025. Huu ni uhaini,” amesisitiza.

IGP Wambura amewaonya watu hao kwamba wakome na wasitishe matamshi yao hayo ya kichochezi lakini pili amesema watachukuliwa hatua za kisheria kutokana na uchochezi wanaoufanya na uhaini wanaoupanga kwani vyote ni makosa ya jinai.

Amesema Jeshi la polisi halitakaa kimya na kuwavumilia, kama walidhani lipo kimya litaenda kuwaonesha kuwa halipo kimya kwa yeyote atakayevunja sheria za nchi.

“Pili niwaombe watanzania wawapuuze watu hawa, Tanzania ni nchi ya amani ni nchi salama hawa wasitake kushawishi na kuingiza nchi kwenye machafuko, hatujawahi kufika huko na hatutakaa tufike huko.

“Niwataarifu wachochezi hawa kuwa jeshi la polisi ni imara, wasitikise kiberiti kama waliwahi kutikisa wakaguswa kule nyuma wasiende hatua nyingine, huku wanakoshawishi kwenda ni sehemu mbaya. Ninawaonya wasijaribu tena kuendelea kufanya ushawishi na uchochezi huo,” amesema.

Aidha, amewaomba wananchi wawe watulivu waendelee kuishi kwa amani na utuvuli kama ambavyo ni mazoea, taratibu na desturi za Tanzania.

Ameongeza kuwa jeshi hilo halitakubaliana na aina yoyote ya uhalifu wa aina yoyote kwani walitegemea kama ni malengo ya kisiasa yaende kwenye hoja za kisiasa lakini yasitoke yakarudi kwenye matendo ya kihalifu.

“Maana nimeona na jeshi tumeona maneno ya uchochezi na kutisha na kuanza kuibuka kwenye mitandao ya kijamii na kuweka ushawishi kwa jamii yetu ambayo ni tulivu.

“Aina hii ya uchochezi na kwa hatua waliyofika ni hatua mbaya kwa sababu mikutano ya hadhara haijazuiliwa, lakini tunachozungumza ni matamko, mtu yeyote asijaribu kusogea huko. Kama hajaona mamlaka ya vyombo vya dola basi this time atayaona,” amesema.

Kauli hiyo ya IGP Wambura imekuja siku moja baada ya Wakili Boniface Mwabukusi kutangaza kuwa wataandaa maandamano yasiyo na ukomo nchi nzima iwapo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halitafanyia marekebisho vifungu vya mkataba huo wa bandari ndani ya siku 14.

Jana tarehe 10 Mahakama Kuu kanda ya Mbeya ilitoa huku na kutupa mbali hoja sita muhimu zilizowasilishwa na wakili huyo aliyewakilisha wananchi wane waliofungua kesi ya kikatiba kupinga baadhi ya vifungu vya mkataba huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za SiasaTangulizi

Samia awataka watanzania kudumisha muungano

Spread the loveRais wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kuendeleza Muungano kwa...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

error: Content is protected !!