Sunday , 29 January 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Igalula waomba umeme kupunguza gharama za mafuta mgodini
Habari Mchanganyiko

Igalula waomba umeme kupunguza gharama za mafuta mgodini

Spread the love

MKURUGENZI Mtendaji wa Mgodi wa Igalula uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Hussein Makubi ameiomba serikali kupitia Wizara ya Nishati kuwaletea umeme katika mgodi huo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa madini ya dhahabu kwenye mkoa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Amesema kukosekana kwa umeme katika mgodi huo kumesababisha kushuka kwa uzalishaji wa madini hayo kwani gharama za mafuta yanayotumika kuendeshea mitambo ya uzalishaji ni kubwa ukilinganisha na kupanda kwa bei ya mafuta hayo.

Akizungumza na MwanaHalisi Online jana tarehe 22 Januari, 2023, Mkurugenzi huyo amesema kupatikana kwa nishati hiyo kutaongeza tija kwani wachimbaji wadogo watazalisha zaidi kuliko sasa wanapolazimika kutumia nishati mbadala ya mafuta.

Amesema mbali na mgodi huo wenye takribani ya wafanyakazi zaidi ya 6,000, pia kuna

wachimbaji wadogo ambao pia wanahitaji miundombinu bora ya maji safi na salama, umeme pamoja na barabara ili kurahisisha uendeshaji wa shughuli hizo.

Pamoja na Mambo mengine mkurugenzi huyo amempongeza Waziri wa Madini, Dk. Dotto Biteko kwa usimamizi mzuri wa sekta hiyo na kupunguza tozo mbalimbali ambazo zimefanya wachimbaji kupata nguvu ya kuendelea na shughuli zao na kupata kipato kinachoweza kuendesha maisha yao.

Akizungumzia upande wa utunzaji wa mazingira Mkurugenzi huyo amesema yapo maeneo ambayo ni maalumu kwa shughuli za uchimbaji lakini pia kuna maeneo ndani ya mgodi yameandaliwa kwa ajili ya upandaji wa miti ili kurejesha uoto wa asili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Huawei Tanzania yatajwa miongoni mwa waajiri bora kimataifa

Spread the loveKAMPUNI ya Huawei Tanzania imetajwa kuwa mwajiri bora nchini na...

Habari Mchanganyiko

Waziri wa uchumi wa Finland atua nchini, kuteta na mawaziri 7

Spread the loveWAZIRI wa Masuala ya Uchumi wa Finland, Mika Tapani Lintilä...

Habari Mchanganyiko

Asimilia 79 wafeli somo la hesabu matokeo kidato cha nne

Spread the loveWATAHINIWA wa shule 415,844 sawa na asilimia 79.92 ya watahiniwa...

Habari Mchanganyiko

NECTA yafuta matokeo ya watahiniwa 333 kwa kuandika matusi, kudanganya, 286 yazuiwa

Spread the loveBARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta) leo Jumapili limetangaza kuyafuta...

error: Content is protected !!