Thursday , 28 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Saba wakamatwa tuhuma za mauji ya hakimu Mwakyolo
Habari Mchanganyiko

Saba wakamatwa tuhuma za mauji ya hakimu Mwakyolo

Spread the love

JESHI La Polisi mkoani Mbeya linawashukilia watu saba kwa tuhuma za mauji ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Handeni, Joakim Mwakyolo yaliyotokea katika Kijiji cha Kibole, Kata ya Itete tarafa ya Busokelo, Wilayani Rungwe mkoani Mbeya. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Ambikile Mwakangumbya, Zawadi Mwakagile, Lutengano Mwakaguile, Wito Mwakatobe, Lwitiko Komile, Aliko Mwakikokyo na Ubike Isasa.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga wakati akiongea na waandishi wa habari mkoani hapo.

Kamanda Kuzaga amesema bado wanaendelea na msako wa kuwatafuta wote waliohusika katika mauji hayo na kuonya wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

Itakumbukwa kuwa mauji hayo yalitokea mnamo tarehe 23, Januari, 2023 saa 2 usiku baada ya wananchi kumshambulia Mwakyolo kwa mawe na vitu vyenye ncha kali ambapo inadaiwa kuwa marehemu aliwahi kuwa na mgogoro wa ardhi na wananchi wa Kijiji hicho.

Akielezea kiini cha mgogoro ambao hatimaye umesababisha kifo cha Hakimu huyo kuwa ni mgogoro wa ardhi uliokuwepo baina ya Kijiji hicho na marehemu.

Amesema marehemu alikuwa akishtakiana na wananchi wa Kijiji cha Kibole kuhusu umiliki wa ardhi yenye ukubwa wa hekari 60 ambayo Serikali ya Kijiji kinadai kuwa ni hifadhi.

“Lakini Mwakyolo alidai alinunua eneo hilo kwa mwenyeji wa kijiji hicho,” amesema Kamanda Kuzaga.

Ameongeza kuwa mgogoro huo ulifikia ngazi ya Mahakama Kuu shauri la ardhi namba 8 la mwaka 2018 ambapo Marehemu alikuwa ndiye mpelekea maombi dhidi ya Serikali ya Kijiji cha Kibole.

Amesema shauri hilo liliisha Desemba 2021 ambapo Serikali ya Kijiji na wanakijiji walipata ushindi.

“Lakini mnamo tarehe 20 Januari, 2023 majira ya saa 2 usiku wananchi walimwona Mwakyolo akitoka katika eneo hilo na ndipo walivamia na kumhoji kwanini ameenda katika shamba hilo ilhali haruhusiwi kufika hapo.

Amesema hali hiyo ilisababisha ugomvi baina yao na kusababisha marehemu ambaye alikuwa na bastola kufyatua risasi na kujeruhi wananchi wawili.

“Wananchi waliojeruhiwa ni pamoja na Tubuke Kisasa (48) ambaye alijeruhiwa na risasi eneo la paja na Huruma Mwakakibula (45) ambaye alijeruhiwa na risasi kwenye ugoko wa mguu,” amesema.

Amesema baada ya kujeruhiwa ndipo kundi kubwa zaidi lilimvamia Mwakyolo na mwenzake ambaye hajafahamika na kusababisha mauji yao.

Amesema ukaguzi katika eneo la tukio jeshi hilo lilikuta mawe, bastola pamoja na magazine mbili ambazo hazikuwa na risasi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyabiashara, wawekezaji China waridhia kuwekeza bil. 800 katika sekta 5 nchini

Spread the loveUJUMBE wa wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Jimbo la Changzhou...

Habari Mchanganyiko

Bil. 4.42 kumaliza uhaba maji kata 2 Musoma Vijijini

Spread the loveWANANCHI wa kata za Busambara na Kiriba, Jimbo la Musoma...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Soko nepi za watoto lashuka, watu wazima lapaa

Spread the loveKiwanda cha kutengeneza nepi cha Japan kimetangaza kuwa kitaacha kutengeneza...

error: Content is protected !!