Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara IFC yazindua programu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini
Biashara

IFC yazindua programu ya kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini

Spread the love

SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Benki ya Dunia (IFC) imezindua mpango mpya wa kuwezesha wanawake kiuchumi ujulikanao kwa jina la ‘Anaweza’ ambao utadumu kwa muda wa miaka mitano. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Mpango huu wa ushauri wa miaka mitano una thamani ya dola  za Marekani milioni 10 ukiwa na malengo matatu ambayo ni Kuwezesha upatikanaji wa ajira kwa wanawake na ushiriki wao katika uongozi.

Kkongeza idadi ya wanawake wafanyabiashara na upatikanaji wa huduma za kifedha na zisizo za kifedha kwa ajili ya biashara zinazomilikiwa na wanawake, na kuimarisha biashara za wanawake ziweze kuongeza uzalishaji wa mtaji na kupata masoko katika sekta muhimu kama vile biashara ya kilimo, viwanda, huduma za kidijitali na utalii.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi w IFC Afrika Mashariki, Jumoke Jagun Dokunmu amesema Taasisi hiyo kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania imewekeza kwa akina mama wajasiriamali ili kuwainua kiuchumi.

Katika Uzinduzi huo Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa wanawake wanatakiwa kuwezeshwa kiuchumi ili kuweza kukabilana na changamoto mbalimbali ambazo wanakumbana nazo na kuondokana na unyanyasaji ambao wanakumbana nao .

Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo ambaye ameeleza kuwa kwa sasa wanawake wa kitanzania wapatao asilimia 65 wamekuwa wakichangia kuongeza pato la taifa kwa kuzalisha kupitia biashra zao ndogondogo japo bado wanakabiliana na changamoto mbalimbali za kimtaji.

Hata hivyo, Jumeke ameeleza kuwa Taasisi hiyo imeingia katika programu hiyo ya kuwezesha wanawake kutokana na kuwa nchi ya Tanzania kuwa kati ya nchi ambayo imeweza kutekeleza hali na usawa wa kiuchumi .

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia,Watoto, Wazee na Makundi Maalumu, Dk. Dorothy Gwajima ambaye amemwakilisha Makamu wa Rais Katika Uzinduzi wa Programu hiyo Dk.Philipo Mpango amesema kuwa Tanzania kwa Kushirikiana na IFC itatekeleza mpango huo kwa muda wa miaka mitano.

Dk. Gwajima amesema kuwa akina mama wengi kwa sasa wameboreshewa mazingira ya kujikwamua kiuchumi licha ya kuwa bado kuna mapungufu makubwa katika utendaji wao wa kibiashara kutokana na kuwepo na mazingira magumu ya kimtaji.

Hata hivyo amesema kuwa pamoja na serikali kuendelea kuwaboreshea mazingira ya kuwakwamua kiuchumi lakini ni asilimia 12 tu ya wanawake ambao wanakadi za benki jambo ambalo linaweza kuwanyima fursa ya kupata pesa kupitia taasisi hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!