Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Idadi ya vifo ajali Tanga yaongezeka kufikia 20
Habari Mchanganyiko

Idadi ya vifo ajali Tanga yaongezeka kufikia 20

Spread the love

MKUU wa mkoa wa Tanga, Omar Mgumba leo Jumapili amesema majeruhi watatu katika ajali iliyotokea juzi Korogwe mkoani Tanga, wamefariki dunia na kuongezeka idadi ya vifo vilivyotokana na ajali hiyo kufikia 20 kutoka vifo 17 ambavyo vilitokea siku ya ajali.

Amesema majeruhi hao wawili ni watoto walikuwa wamelazwa katika Hospitali ya Bombo Tanga na mmoja alikuwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mgumba ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Februari 2023 wakati akizungumza katika ibada ya kuaga miili 20 iliyofanyika katika Hospitali ya Magunga Korogwe mkoani Tanga.

“Jana tulikuwa na vifo 17 vilivyotokana na ajali hii na kimoja cha mzee Athanas Mrema kwa hiyo jumla tulikuwa na miili 18.

“Katika wale majeruhi wetu 12 tuliwahamishia hospitali ya Bombo na wawili tuliwahamishia Muhimbili ambapo sasa mmoja amefariki, lakini wale watoto tuliowahamishia Bombo, wawili nao wamefariki.

“Ajali hii sasa sio watu 17 ni watu 20, na marehemu inakuwa ni watu 21. Hawa watoto wawili tuliona ni busara nao tuwaandae vizuri kwenye hospitali ya Bombo, tunawaaga wakati mmoja hapa,” amesema.

Amesema mmoja aliyefariki katika Hospitali ya Muhimbili atasafirishwa kupelekwa Marangu kwa maziko.

Ameongeza kuwa kwa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan mbali na viongozi wa mkoa huo kushiriki msiba huo, mkoa utabeba gharama za msiba huo ikiwamo kusafirisha miili hiyo hadi itakapohifadhiwa katika nyumba zao za milele.

Ajali hiyo ilitokea tarehe 3 Februari 2023 muda wa saa 4:30 usiku, eneo la Magila Gereza, katika barabara ya Segera – Buiko, ilihusisha gari aina ya Fuso na basi dogo aina ya Toyota Coaster, iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Basi hilo, lililokuwa na abiria 26, lilikuwa limebeba mwili wa Athanas Cosmass Mrema, aliyefariki dunia katika hospitali ya Bochi – iliyopo Kwa Msuguri katika Kata ya Saranga – Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!