Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Herbinder Seth, Rugemarila waiangukia mahakama
Habari Mchanganyiko

Herbinder Seth, Rugemarila waiangukia mahakama

Herbinder Seth na mwenzake James Rugemarila wakitinga mahakamani
Spread the love

TANGU Julai 2017, mpaka leo bado upelelezi haujakamilika, tunaomba upelelezi ukamilike ili tujue mwisho wake ni nini. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Hayo ni madai ya upande wa utetezi kwenye kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Herbinder Seth na mwenzake James Rugemarila katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa upande wa utetezi Michael Ngalo amedai haya leo tarehe 17 Januari 2019 mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina.

Wakili Ngalo ameomba upelelezi wa kesi hiyo ukamilike ili wajue mwisho wake ni nini kwani washtakiwa hao wapo gerezani tangu Julai 2017.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai ameeleza mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine ili kukamilisha upelelezi huo.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mhina aliharisha kesi hiyo hadi Januari 31,2019 kwa ajili ya kutajwa.

Rugemarila na Seth mwenzake wanakabiliwa na mashitaka 12 ya uhujumu uchumi kwa kula njama, ya kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya dola za Marekani 22, 198,544.60 na Sh. 309,461,300,158.27.

Washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Oktoba 18, 2011 na Machi 19 , 2014 jijini Dar es Salaam walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ili kutenda kosa.

Inadaiwa katika mashitaka ya kujipatia fedha a kati ya Novemba 28 na 29, 2011 na Januari 23,2014 katika Makao makuu ya Benki ya Stanbic Kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi la Mtakatifu Joseph, kwa ulaghai washitakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh 309, 461,300,158.27.

Pia washitakiwa wote wanadaiwa kuisababishia serikali hasara ya Sh. 309,461,300,158.27. wanadaiwa kutenda makosa hayo Novemba 29, 2013 katika Benki ya Stanbic tawi la kati kinondoni, kwa vitendo vyao waliisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 22, 198, 544.60.

Kati ya Novemba 29,2013 na Januari 23, 2014 maeneo tofauti Dar es Salaam kwa pamoja walitenda kosa la kutakatisha fedha kwa kuchukua fedha kutoka BoT ambazo ni dola za Marekani milioni 22.1 na Sh. 309.4 bilioni wakati wakijua fedha hizo ni zao la kujihusisha na genge la uhalifu.

Washitakiwa wapo rumande kwa kuwa mashitaka hayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

Habari Mchanganyiko

Kairuki awaweka mtegoni wakurugenzi watakaoshindwa kufikia malengo ya makusanyo

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na...

error: Content is protected !!