Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Haya hapa majina wafanyabiashara 13 waliofariki ajalini Songea
Habari Mchanganyiko

Haya hapa majina wafanyabiashara 13 waliofariki ajalini Songea

Spread the love

 

JESHI la Polisi wa Mkoa wa Ruvuma limetaja majina ya wafanyabiashara 13 waliofariki dunia katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia jana tarehe 10 Aprili 2023 baada ya gari aina ya Mitsubishi Fuso walilokuwa wakisafiria kutumbukia katika daraja la Mto Njoka Namatuhi lililopo barabara ya Ndongosi – Namatuhi, Songea vijijini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Ruvuma … (endelea).

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Marco Chilya amesema gari hilo lenye namba za usajili T800 BXB, lililokuwa likiendeshwa na Thobias Njovu, liliacha njia na kutumbukia mtoni mara baada ya kushindwa kupanda Mlima.

Aidha, Kamanda Chilya amewataja waliofariki kwenye ajali hiyo ambao wengine walifahamika kwa jina moja kuwa ni Happy Msemwa, Jafari Ngalimus, Hidaya Salum, Biesha Yahaya, Mustafa Ally, Mwaisha, Hamad, Juma Said, Boniface na Christofa Msuya.

Wengine ni Deograsia Mapunda, Simba na mama Faraja huku akiwataja majeruhi kuwa ni Hamis Mbawala na Christofa Banda na wamelazwa katika kituo cha afya cha Mpitimbi na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Songea.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!