Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Hatma ya Aveva na mwenzake Ijumaa
Habari Mchanganyiko

Hatma ya Aveva na mwenzake Ijumaa

Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga kutolea uamuzi juu hatma ya dhamana ya aliyekuwa Rais wa klabu ya Simba, Evance Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange (Kaburu) baada ya upande wa Serikali kuiarifu mahakama hiyo nia ya kukata rufaa kupinga uamuzi wa kufutiwa kwa makosa ya utakatishaji fedha. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).

Tarehe 19 Septemba, 2019, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliamua kufuta mashtaka yote ya utakatishaji fedha kwa watuhumiwa hao ambapo siku ya pili yake Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DPP) kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliijuza mahakama hiyo kuwa (DPP) anania ya kukata rufaa.  

Mshtakiwa mwengine kwenye kesi hiyo ni Zakharia Hanspope  ambaye hajashtakiwa kwenye makosa ya utakatishaji fedha.

Leo Tarehe 23 Upande wa Serikali imewasilisha hoja juu ya kwanini wanapinga uamuzi huo ambapo Wakili Wankyo amedai mahakamani hapo kuwa kwa mujibu wa sheria DPP akitoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa  Mahakama kuu rufaa inakuwa tayari.

Ameiomba mahakama hiyo kusimamisha dhamana za washtakiwa hao mpaka rufaa hiyo itakaposikilizwa kwa kuwa zinatokana na kufutwa kwa mashtaka ya utakatishaji fedha ambapo upande huo umeeleza kufutwa kwa makosa hayo ndiyo kumelekea kupatikana kwa dhamana.

Baada ya hoja hizo Wakili wa Utetezi, Nehemia Nkoko amedai mahakamani hapo Upande wa Mashtaka haujapinga dhamana ya washtakiwa hao na kwa kuwa mahakama hiyo ilishatoa dhamana kwa watuhumiwa hao  haoni sababu ya kuzuiliwa.

Hakimu Simba ameahilisha shauri mpaka tarehe 27 Septemba mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi juu rufaa hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!