Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Zitto ‘afukua makaburi’ Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Zitto ‘afukua makaburi’ Chadema

Spread the love

ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, amezungumzia tukio la kutimuliwa kwake ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwamba lilimpa hamasa. Anaripoti Regina Mkonde…(endelea).

Amesema, alijiunga na siasa (Chadema) akiwa na umri wa maiaka 16 na hata alipofukuzwa kwenye chama hicho, hakukata tamaa na kaumua kaunzisha ACT-Wazalendo.

“…Nilijiunga na chama cha siasa kwa mara ya kwanza nikiwa na umri wa miaka 16, chama cha Chadema. Nilipofukuzwa chama hicho nikashirikiana na wenzangu kuanzisha chama cha ACT. Sikukata tamaa kwani niliamini kuwa ile ni mitihani ya maisha, ni kukomazwa,” amesema Zitto.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini ameandika maneno hayo leo tarehe 24 Septemba 2019, katika ukurasa wake wa Twitter akiwa kwenye kumbukizi yake ya siku ya kuzaliwa akifikisha miaka 49.

“Leo nimefikisha umri wa miaka 49…. Leo ninaongoza chama kinachokuwa kwa kasi kuliko vyama vyote nchini. Mungu ni Mkubwa.

Hata hivyo, mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea, ameliambia MwanaHALISI Online, kuwa kwa ufahamu wake, Zitto hajawahi kufukuzwa Chadema.

“Zitto Zuberi Kabwe, kwa ufahamu wangu na weledi wangu, hakuwahi kufukuzwa uwanachama ndani ya Chadema. Alijifukuzisha. Alikwenda kinyume na Katiba ya chama chake.”

“Kwamba, Katiba ya Chadema, inazuiwa wanachama wake kwenda mahakamani. Zitto alikwenda mahakamani kupinga kuhojiwa na Kamati Kuu (CC) ya chama chake, kuhusiana na madai ya kutaka kumuondoa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kinyume na taratibu.

“Hivyo basi, kwa maamuzi yake hayo, Zitto akawa moja kwa moja amejifukuzisha chama,” amesema Kubenea.

Alipoulizwa kuwa kwa maoni yake yeye binafsi, anakubaliana na kuwapo kwa katazo hilo la kikatiba, Kubenea amesema, “sikubaliani nalo: na kuongeza;

“Kwa chama cha siasa kinachoamini kwenye utawala wa sheria na demokrasia, kuzuia wanachama wake kwenda kuhoji maamuzi yake mahakamani, siyo jambo jema.”

Zitto alikimbilia mahakama Kuu Kanda, Dar es Salaam kufungua kesi dhidi ya Chadema akipinga uamuzi wa chama hicho kutaka kumfukuza uanachama. Tarehe 10 Machi 2015, mahakama hiyo ilitupilia mbali maombi yake.

Tundu Lissu, Mwnasheria Mkuu wa Chadema ndiye aliyetangaza uamuzi wa chama hicho kumvua uanachama rasmi Zitto, kwa maelezo kwamba kanuni na sheria za chama hicho zinakataza mwanachama kushitaki chama hicho mahakamani.

Ndani ya Chadema, Zitto alishika nafasi kadhaa ikiwemo Ukurugenzi wa Mambo ya Nje mwaka 2004 na Mkurugenzi wa Uchaguzi na Kampeni, mwaka 2005 alichaguliwa kuwa Katibu wa Wabunge wa Chadema baada ya kuteuliwa kuwa mbunge na mwaka 2007 alichaguliwa na Baraza Kuu la Chadema kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara, nafasi aliyoshikilia hadi alipofukuzwa uanachama wa chama hicho.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

error: Content is protected !!