August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hatima ya uchaguzi TLS kutolewa leo

Tundu Lissu, Mgombea wa Uenyekiti wa TLS (katikati). Kulia ni Lawrance Masha. Kushoto Katibu Mkuu wa Chadema, Vincent Mashinji

Spread the love

MAWAKILI wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) kimeiomba Mahakama Kuu ya Tanzania kutupilia mbali kesi ya Kikatiba ya kupinga kanuni za uchaguzi iliyofunguliwa na mwanachama Onesmo Mpinzila, anaandika Faki Sosi.

Mlalamikiwa kwenye kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na wengine waliiomba kuunganishwa kwenye kesi hi pamoja na mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha na Jamhuri Johnson.

Kesi hiyo imeeitwa mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Rose Temba kwa ajili ya kusikilizwaji maombi ya kuunganishwa kwa Lissu na wenzake.

Awali upande wa wadaiwa wakiongozwa na wakili Sinare Zaharani waliibua hoja za pingamizi za madai hayo.

Kuanzia saa 7:10 mchana hadi saa 1 usiku jana shauri hilo lilisikilizwa mbele jaji kiongozi Rose Temba, mawakili wa TLS waliomba mahakama kesi hiyo itupwe kutokana muombaji kuwa hana leseni ya sharia.

Zaharan alieleza kuwa mleta maombi (Mpinzila) hana mamlaka ya kisheria kufungua kesi hiyo. Pia katika kiapo chake hakuna sehemu yeyote aliyoonyesha kuwa ni wakili wala mwanachama wa TLS.

Aidha kiapo chake kina hoja za kisheria tu, bila kuwa na maelezo hivyo kina mapungufu ambapo ameomba kiapo ama aya zenye hoja za kisheria ziondolewe.

Naye wakili Jeremiah Mutabyesa alieleza kuwa kesi za Kikatiba hazitakiwi kufikishwa mahakamani moja kwa moja kama kuna njia nyingine za ufumbuzi.

Alieleza kuwa Mpinzila alikuwa na nafasi ya kutoa hoja zake kwenye mkutano wa TLS utakaofanyika Machi 18,mwaka huu jijini Arusha kabla ya kukimbilia mahakamani.

“Hivyo kwa hiki alichokifanya sio sahihi bali alikuwa na nafasi ya kutafuta namna nyingine,” amedai.

Kutokana na mvutano wa hoja za kisheria kutoka kwa Mawakili wa serikali na wa Mpinzila, leo mahakama inatarajia kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Shauri la msingi, Mpinzila amefungua kesi hiyo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na TLS akipinga mambo mbalimbali ikiwemo kanuni ya uchaguzi ya TLS ya mwaka 2016 ambayo inatoa muongozo na sifa za wagombea na jinsi ya kuendesha uchaguzi.

Kwa mujibu wa mdai kanuni hizo zimesainiwa na kutangazwa kwenye gazeti la serikali na mtu ambaye hana mamlaka ya kufanya hivyo.

error: Content is protected !!