Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgombea TLS: Lissu hatatuvuruga
Habari Mchanganyiko

Mgombea TLS: Lissu hatatuvuruga

Meza ya Hakimu
Spread the love

WAKILI Victoria Mandari, ambaye ni miongoni mwa wagombea wa Urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amesema anaamini wagombea wa nafasi hiyo ambao ni wanasiasa hawataingiza maslahi ya vyama vyao iwapo watashinda, anaandika Charles William.

Akizungumza mapema leo asubuhi katika kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, Victoria amesema TLS inaendeshwa kwa kanuni na taratibu zake na hivyo kumekuwepo wa hofu kuwa wagombea ambao ni wanasiasa wanaweza kuivuruga TLS.

“Watu wamekuwa na hofu, ya kwamba iwapo wanasiasa wataiongoza TLS basi watashindwa kutenganisha maslahi ya vyama vyao lakini nadhani TLS ni taasisi imara yenye kanuni zake na kila kiongozi atatakiwa kuzifuata,” amesema.

Victoria ameeleza kuwa uchaguzi wa TLS mwaka huu umekuwa na hamasa kubwa zaidi kutokana na uwepo wa wagombea ambao ni wanasiasa, waliowahi kuwa watumishi serikalini pamoja na mawakili wakongwe.

“Chama chetu kipo tangu mwaka 1954 na kimekuwa kikifanya chaguzi tangu miaka hiyo, lakini mwaka huu kumekuwa na hamasa na msisimko zaidi,” amesema.

Victoria amesisitiza kuwa ingawa yeye ni mgombea pekee mwanamke kati ya wagombea watano na pia hajulikani ni mwanachama wa chama gani cha siasa lakini hatatumia mambo hayo kama vigezo vya kuombea kura.

“Sihitaji kura za huruma, mawakili wanawake ni wengi lakini sitaomba kura za wanawake, kwasababu sigombei kwenda kutetea maslahi ya wanawake bali maslahi ya mawakili wote hapa nchini,” amesema.

Wagombea watano waliopitishwa na kamati ya uchaguzi  ya TLS ni Tundu Lissu ambaye ni Mbunge na Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni, Lawrance Masha ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika serikali ya awamu ya nne, Godwin Mwapongo ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, Francis Stolla ambaye ni Rais wa TLS anayegombea kutetea kiti chake na Mwanamama Victoria Mandari.

Uchaguzi wa TLS unatarajia kufanyika Jumamosi ya tarehe 18 Machi mwaka huu, katika Ukumbi wa AICC, Arusha ambapo mawakili wote hapa nchini watapata nafasi ya kupiga kura ya kuchagua viongozi wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!