Friday , 2 June 2023
Home Kitengo Michezo Habib Kyombo afuzu majaribio Mamelodi Sundowns
Michezo

Habib Kyombo afuzu majaribio Mamelodi Sundowns

Habib Kyombo
Spread the love

MSHAMBULIAJI wa Singida United na timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 23, Habib Kyombo amefuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Mamelodi Sundowns inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mshambuliaji huyo ambae alianza kukipiga kwenye kikosi cha Mbao FC katika msimu wa 2016/17 na kuibuka kuwa mfungaji bora wa kombe la Shirikisho na baadae kutimkia kwenye klabu ya Singida United jana alifanya vipimo vya afya na kufanikiwa kufuzu na kilichobaki ni kumalizana maslahi binafsi.

Septemba 2, 2018 mshambuliaji huyu alipata mwaliko wa kwenda kufanya majaribio ya siku 10 ndani ya klabu hiyo iliyopo kwenye mji wa Pretoria nchini Afrika Kusini na klabu hiyo kufikia maamuzi ya kumsajiri.

Kufanikiwa kwa mshambuliaji huyo kucheza Ligi Kuu Afrika Kusini kutaongeza idadi ya wachezaji raia wa Tanzania ambao wanacheza soka la kulipwa nje ya mipaka ya nchi hii na kuungana na wachezaji kama Simon Msuva, Mbwana Samatta, Himid Mao, Abdi Banda na Hassan Kesi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love  UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei...

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

error: Content is protected !!