Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Wafanyakazi Bandari wafikishwa mahakamani Kisutu
Habari Mchanganyiko

Wafanyakazi Bandari wafikishwa mahakamani Kisutu

Spread the love

WAFANYAKAZI tisa wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na kesi tatu tofauti dhidi wizi wa mali iliyokuwa safarini na utakatishaji wa zaidi ya Sh. milioni 277. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika kesi ya kwanza washtakiwa walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi, aliwataja washtakiwa hao ni Naushad Mohamed, Alfred Mhina, Joseph Mrema, Justine Mosha, Anuary Shampoo na Pius Nyeregeti.

Kishenyi alidai kati ya Agosti 30 na Septemba 9, mwaka huu, washtakiwa walikula njama ya kuiba mali iliyokuwa ikisafirishwa.

Katika shtaka la pili ilidaiwa Septemba 8, 2018 katika geti namba tano la TPA lililopo Wilaya ya Temeke, mshtakiwa Nyeregeti, alijitambulisha kama Nassoro Mohamed kwa Gaspa Swai ambaye ni Ofisa wa TRA, huku akijua siyo kweli.

Katika shtaka la tatu, watuhumiwa hao waliiba kontena lenye nguo zenye thamani ya Sh. 177,608,761 mali ya Nkonde Bright ambayo iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka, Zambia.

Aidha, washtakiwa hao wanadaiwa kujihusisha katika muamala uliohusiana na wizi wa nguo hizo, huku wakijua kuwa mali hiyo ni zao la kosa la utangulizi la mali isafirishwayo

Katika kesi ya pili, ilidaiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde, ambapo Wakili wa Serikali, Eric Shija, alidai Septemba 18, 2018 washtakiwa Anuary Shapoo, Pius Nyeregeti, Athanas Nsenye, Yusuph Mkuja, na Ismail Hajji, walikula njama ya kuiba mali iliyokuwa ikisafirishwa.

Katika shtaka la pili, ilidaiwa washtakiwa waliiba kontena lililokuwa na magunia 520 ya mahindi yenye thamani ya Sh. 31,698,411 mali ya Brian Mwacha ambayo ilikuwa ikisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Zambia.

Pia washtakiwa hao wanadaiwa kubadilisha magunia hayo na fedha kwa kuyauza huku wakijua kuwa kosa hilo ni zao la kosa la utangulizi la wizi wa mali isafirishwayo kwa dhumuni la kupotezea uhalisia wa mali hizo.

Katika kesi ya tatu, mbele Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando, upande wa Jamhuri ulidai kuwa washtakiwa walikula njama ya kuiba kontena lililokuwa na mifuko 520 ya HDPE yenye thamani ya Sh. 68,708,377 mali ya Evatisto Musonda.

Pia imedaiwa washtakiwa hao walibadilisha mifuko hiyo ya HDPE kuwa fedha, huku wakijua mali hiyo ni zao la kosa la wizi wa mali iliyokuwa ikisafirishwa kwa lengo la kupotezea uhalisia wa fedha hizo.

Hata hivyo, washtakiwa walikana mashtaka yao kwa nyakati tofauti na walirudishwa rumande kwa kuwa makosa ya utakatishaji hayana dhamana.

Upelelezi wa kesi hizo haujakamilika na zimepangwa kutajwa tena Desemba 12, mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

Habari Mchanganyiko

Kairuki awaweka mtegoni wakurugenzi watakaoshindwa kufikia malengo ya makusanyo

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na...

error: Content is protected !!