JAJI wa Mahakama Kuu, Sam Rumanyika, ametupilia mbali, mapingamizi ya serikali yaliyolenga kumzuia Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko, kutoka gerezani. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Washinda pingamizi lao mahakamani, kesi yao kuanza kunguruma mchana huu. Mawakili wa serikali hoi.
Kufuatia uamuzi huo, Jaji Rumanyika amepanga kuanza kusikiliza shauri la msingi leo Ijumaa, kuanzia saa nane mchana.
Mbowe na Matiko, waliwasilisha mahakama kuu maombi ya rufaa, kupinga uamuzi wa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri wa kuamua kuwafutia dhamana.
Hakimu Mashauri alichukua uamuzi wa kuwafutia dhamana Mbowe na Matiko, tarehe 23 Novemba. Alidai washitakiwa wamekiuka masharti ya dhamana na wameidharau mahakama.
Akisoma uamuzi wake huo, mbele ya mamia ya wananchi waliokuwa wakifuatilia shauri hilo,
Jaji Rumanyika, alisema kuwa “pingamizi zilizowekwa na serikali hazina msingi.”
Pingamizi hizo ziliwasilishwa juzi mchana na upande wa mashitaka, ukieleza kuwapo mapungufu kadhaa katika maombi ya washitakiwa ya kutaka kurejeshewa dhamana zao.
Miongoni mwa hoja zilizotolewa na upande wa mashitaka, ni kuwa upande wa utetezi, umekosea kwa kutumia kifungu cha sheria Na. 359 na 361 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kuwasilisha rufaani yao.
Madai hayo yalipingwa na mawakili wa utetezi, Dk. Rugemeleza Nshalla, Peter Kibatala na Jeremia Mtobyesa.
Mbela ya Jaji Rumanyika, mawakili hao walisema, hoja hiyo iliyowasilishwa na wakili mwandamizi wa serikali, Faraja Nchimbi, mepitwa na wakati kwa mujibu wa sheria.
Leave a comment