Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Forbes yamtaja tena Dk. Samia miongoni mwa wanawake 100 wenye uwezo mkubwa duniani
Habari MchanganyikoTangulizi

Forbes yamtaja tena Dk. Samia miongoni mwa wanawake 100 wenye uwezo mkubwa duniani

Rais Samia Suluhu Hassan
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan ametajwa na jarida la Forbes kwa mwaka wa pili mfululizo kuwa miongoni mwa wanawake 100 wenye ushawishi, nguvu na uwezo mkubwa wa uongozi duniani katika orodha ya 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Rais Samia ametambuliwa katika orodha hiyo ambayo pia amejumuishwa na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, Rais wa Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya, Christine Lagarde na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Kristalina Georgieva, na aliyekuwa mke wa mmoja wa watu matajiri zaidi duniani Jeff Bezos, Mackenzie Scott. nao pia wametambuliwa kwenye orodha hiyo inayoheshimiwa duniani.

Leyen ameshika nafasi ya kwanza katika orodha hiyo ya mwaka huu, wakati Samia yuko nafasi ya 95.

Kwa upande wake, Rais Samia ambaye mwaka jana alishika nafasi ya 94 kwenye orodha hiyo ya Forbes ya wanawake wenye nguvu zaidi duniani, amejipatia sifa kutokana na uongozi wake shupavu kwenye kukabiliana na janga la corona nchini Tanzania tangu aingie madarakani Machi 2021.

Hayo yanajiri baada ya Benki ya Dunia hivi karibuni iliipongeza serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia kwa “miujiza ya kiuchumi” kutokana na kuweza kudhibiti mfumuko wa bei wakati nchi nyingi duniani zinakabiliwa na janga la uchumi kutokana na vita ya Ukraine.

Rais Samia ameelezwa na wachambuzi wa siasa na uongozi nchini na wa kimataifa kuwa huenda akaweka historia ya kuwa mmoja wa viongozi mahiri siyo barani Afrika tu, bali duniani kote.

Tangu aingie madarakani, Rais Samia ameongeza uwekezaji wa serikali kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ya miundombinu na amewekeza pesa nyingi kwenye sekta za maji, elimu na afya.

Katika nyanja ya elimu, alipoingia madarakani, serikali ilikua inatoa elimu bure hadi kidato cha nne, lakini akaongeza elimu bure hadi kidato cha sita.

Rais Samia pia ameonesha umahiri wa uongozi kwa kuongeza makusanyo ya kodi na kuifanya Tanzania ing’are kwenye nyanja ya diplomasia na mahusiano ya kimataifa.

Samia amepongezwa pia kwa kuleta utulivu wa kisiasa nchini na kwa kuagiza serikali yake ianze mchakato wa kuleta mageuzi ya haki za jinai.

Rais Samia ameanzisha mazungumzo na viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na kuunda kikosi kazi ambacho, pamoja na mambo mengine, kimependekeza mageuzi makubwa ya sheria za uchaguzi nchini na kukamilishwa kwa mchakato wa katiba mpya.

Samia pia amerejesha imani ya wafanyabiashara na wawekezaji wa nje na ndani kwa Tanzania, ikiwemo kufanya mazungumzo na tajiri mkubwa zaidi Afrika, Aliko Dangote, na kuanzisha majadiliano na makampuni makubwa ya nishati duniani ambayo yanapanga kuwekeza zaidi ya Shilingi trilioni 90 kujenga kiwanda cha kuchakata gesi asilia (LNG) nchini.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!